Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Watoto katika hatua zao za ukuaji na kujifunza wanakuwa na mambo flani flani ya kufurahisha sana yaani mwanao anaweza kukuvunja mbavu balaa.

Mfano

1. Mwanangu (1.5years) anaweza kuwa anatazama TV akisikia unaongea na simu au umeweka music kwenye simu anakimbia kuja kuangalia simu hata kama TV ilikuwa na TV program ya katuni nzuri kiasi gani[emoji23] [emoji23] [emoji23]

2. Ukitaka alale we nenda kitandani weka music kwenye simu yako atakuja mwenyewe hata kama alikuwa anakwepa kulala[emoji23]

3. Anaheshimu simu yangu kama kituo cha polisi ila ya mama yake kashaipasua ukiiona utajua mama yake anafanya kazi idara ya miamba (geology)[emoji23]

4.Kupenda safari akiona mtu anatoka tu anaanza kuaga bye bye akijua nayeye anahusika na safari[emoji23] [emoji23]

5. Chakula kikiwa tayari, kabla sijaitwa kula yeye akiona mambo yako tayari anakuja kunipigapiga mgongoni(hajajua kuongea) akiashiria msosi tayari basi ukipotezea anaenda anarudi mpaka utakapoinuka[emoji23] [emoji23]

6. Mwanangu anatabia flani kama wivu, akiona naongea na mama yake mara nimemshika mkono tunaongea kama jambo la siri anakuja fasta analia anataka mama yake ambembe[emoji23]. Nadhani hajajua kwamba mama yake ni mke wangu[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Hivi ni baadi ya vituko vya watoto mdau ongeza vya mwanao

Watoto wanaleta raha sanaaa
Malezi mengine mpaka najisikia vibaya nikisoma Watu wanavyoishi na watoto wao. Yani mtoto nimwambie fanya kitu flani akatae au nimkataze usifanye kitu flani halafu aendelee kufanya, then nimchekee niseme anamsimamo Hataki. Ninachapa kwa waya wa Redio au mkanda, na nikiongea kitu mara moja kisirudiwe tena na wanajua vema taratibu zangu.

Acheni kulea watoto kama mayai, mtoto anapaswa kuwa na heshima na adabu, akikosa muadhibu na akifanya vizuri mpongeze. Mnatengeneza jamii ya hovyo sana Kwa kuchekea upuuzi wa Watoto, Mtoto anapaswa akikuangalia usoni ajue Hilo jambo sio zuri na hujapenda na aache mara moja.

Haya Maisha yenu ya kizungu yanipitie mbaalii kabisa
 
Mie wa kwangu Ana miaka minne wa kike. Bado Ana tabia ya kunifuata kila ninapopenda nikiwa nyumbani nafanya kazi zangu.

Sasa juzi kati hapo nikawa namwambia dadaake umeiona nimeota mkia yaani ile kuwa ananifuata nyuma kila wakati.

Sasa yeye anashangaa imekuaje mie binaadam halafu nimeota mkia.

Kuna muda nimesimama naona ananipandisha nguo.... Nikamyakia wee vp unataka nini.... Ndio ananambia nataka niuone huo mkia uloota. Ddduh nikasema hii sasa kazi. Yaani wtt wanajifunza na ku observe fasta
 
Hahahaha
 
bila picha za watoto ni chai,wengi tunasimulia stori za watoto wa kaka zetu na shemeji zetu...
Mi mtot wa kaka angu ana miaka 3 wa kiume korofi balaa mda mwingine ananiambia ondoka kwenu hapa kwa baba angu mara achia rimoti,yaan kama unafatilia vipindi vzur utasubiri katuni ziishe....nami nshasema siondki hapa maan maisha bdo yapo tight
Ngoja nifagie banda la kuku kwanza
 
1. Wa kwangu ana 1.9 akiwa na kiu anakuja anakushika mkono anakuvuta mpaka kwenye fridge ole wako ukamchukulie maji ya moto pembeni kilio chake kama filimbi, nimegundua mbinu juu ya fridge naweka jagi la maji ya kawaida akinipeleka kwenye fridge nafungua natoa jagi naweka juu ya fridge kenyewe kafupi juu kwa juu na kabadilishia jagi kakinywa sio ya baridi kanasita kama hakajaridhika afu kanakunywa kishingo upande.

2. Kanapenda kuchezea remote ya TV kanatoa betri ole wako urudishe betri unalo hilo mpaka kamepoteza remote kubadili channel tunafanya kubadilishia kwenye kingamuzi.

3. Kamjamaa kana penda kulala karibu na feni ukikasogeza pembeni kanarudi karibtt na feni sasa umeme ukikatika mnalo, kajamaa hakaelewi kitu ni kilio.

3. Kuna baadhi ya matangazo ya biashara kamjamaa kakisikia hata kama kako nje kanacheza katakuja speed kuja kuangalia tangazo likiisha kwa unyongeee kanatoka nje kujumuika na wenzake kucheza.

4. Kajamaa hua kanakua na itikadi za kibabe, kakiona namkumbatia mama yake kanakuja kanamind basi katafanya kila aina ya uayawani wake ilimradi nimuachie mamake.

5. Ukikanunulia pipi (japo nadra sipendelie kumpa ila kanapenda balaa) kakiwa kanalia basi naenda nako dukani kukanunulia, bwanae nunua moja ukisema ununue mbili nyingine utampa badae ye anataka ufungue zote umpe alambe huku kisha huku.

6. Kamjamaa kakivalishwa viatu tu kanajua kuna mtoko, sasa mvalisheni viatu afu muendelee kujichelewesha, kanakufuata kanakushika mkono kanakuvuta mpaka mlangoni afu kanaanza kuguna guna

7. Kajamaa ni kadogo ila kanajua ninapomfokea mama yake kanapoteza furaha mda mwingine kanaenda kujificha chini ya meza haa ha.

8. Kupanda juu ya vitu. Juu ya meza juu ya kinanda changu. Afu akisha panda juu anakojoa aftt anashuka mpaka kamearibu kinanda changu kamekikojolea mpaka kimepata circuit imepiga shoti.

Aise watoto ni faraja sana sana.
Mungu akuongezee na vingine vingi vya aina hiyo, vingine vije kuwa vi-Samia Suluhu Hassani, na vingine vi-Hussein Mwinyi
 
bila picha za watoto ni chai,wengi tunasimulia stori za watoto wa kaka zetu na shemeji zetu...
Mi mtot wa kaka angu ana miaka 3 wa kiume korofi balaa mda mwingine ananiambia ondoka kwenu hapa kwa baba angu mara achia rimoti,yaan kama unafatilia vipindi vzur utasubiri katuni ziishe....nami nshasema siondki hapa maan maisha bdo yapo tight
Ngoja nifagie banda la kuku kwanza
Ila watu hahahhahahahahahaa
Mada kama hii huwa zinaletwa na wanawake halafu wanaume ndio wanachangia.

Sasa kidume mzima unajipinda unaanzisha uzi kama huu....!!!!

Unatukosea sana wanaume wenzako.
ishii we vipi.
 
Nina mdogo wangu ana 3yrs Ke, she'svery smart aisee.. Ukimwita mtoto hataki anasema yeye ni mkubwa (kaanza kuongea ana miezi 8. Kaacha ziwa na waka 1.
Very bold and strong, anakwambia yeye hatakuja kuolewa.
Anaimba Yope yote na kuicheza.
Namkubali alivyo intelligent, nadhani atakua smart kuliko watoto wote nyumbani
Hii dunia huu. Baba unajisifu mwanao anajua kuimba yopee. Aiseeee
 
Mimi ninao wanne. Wakike 3 na kiume 1. Wakike mkubwa alipokuwa ana miaka 6 alikuwa hakuwahi kuona mtu kabla hijabu na Nikabu. Siku 1 tulienda Morogoro kwa Bibi yake, tukaona anakuja mbio ndani, tukimuuliza nini? Akasema Jiniii yupo nje. Kwenda kuangalia ni mama mmoja wa kianswar Sunna Jirani yetu.

Niliona aibu na nikajua leo tunapigwa kamwe na wajahidina. Ikabidi nikae nae ndani na kumfundisha kuhusu huyo mama na uvaaji.
 
Wangu amelelewa na mam ake na wajomba zake bas anadeka kishenzi huwa nikamuoji oji maswal kadha unamuona anaanza kudondosha machozi Bila kupigwa bas namuita mam ake aje hapo mnk wakt nikimuoji oji sitaki mama ake awe Hapo bas mm namuita mama ake aje amuone mwanae anayelia Bila kupigwa mma ake anamuuliza unalia nn j..bas mtot haseme kitu analia tu bas anajikuta nimemkamata na kumpiga kisawasawa na kumvinya haswa had karibu kutoa nyama yaani ananiudhi Sana baas analia sanaaa baadae tunambebeleza anasepa zake mm hapo saa hyo lawama zote nimeshamuangushia mama ake
Huku nimeacha hell kidgo usku utaona mma anapiga simu tunaongea nae namchekesha kumsahaulisha ukatili wangu dhid yake bas nampongeza na kuahidi kumnunulia zawad nzuri akifanya vzr Zaid shuleni bas anafurahi utasikia anakuaga usku anasema usiku mwema baba mungu akubariki .

Ila hapo nasem kimoyomoyo huyu mtot anadeka Sana baadae kuchunguza naaambiwa huyu mtot anadeka kwa kuwa Hana mdgo wake inabidi atafutie mdg wake nikasema Nani azae na hyu mam Tena mm kbsa nakuja kuanza kumchakt mam ake hpn acha abaki single mam tu atafute mtu mwingine was kumpa watot ila Simon mm
 
Sasa mtoto amekukosea nini??? Jamani
 
Nimetoka safari kama miez 4 hivi imepita sijaonekana, mwanangu wa kike wa miaka 2 anafurahi sana kuniona home na vizawadi vyake. Ananiuliza baba vipi hujapata ajali maana jana kwenye TV imetokea ajali, Namjibu namshukuru Mungu nimefika salama, Anashagaa hee kumbe na huko ulikokuwepo kuna Mungu? Hahahaahh..
 
Back
Top Bottom