Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Mwanangu wa 3 ana umri wa miaka 6 hivi....,,week iliyopita nilimnunulia FIRIMBI,,,aisee hatukulala siku hyo....hadi Tisa za usiku ANAPIGA FILIMBI TU...hatukulala siku hiyo ni KELELE ZA FIRIMBI USIKU MZIMA,,,ikabidi niichukuwe nikaiweka chumbani kwangu,,,ALFAJIRI SAA KUMI NA MBILI,,,,,nasikia MTU anagonga mlango,,kufunguwa ni yeye,,,anataka FILIMBI YAKE,,,aisee ZILIPIGWA FILIMBI MFULULIZO HADI NIKAJUTA KUMNUNULIA FIRIMBI,,...duu...tuliendelea KUPATA ADHA YA KELELE ZA FILIMBI hadi tulipoamua KUPANGA MATOKEO YA KUIFICHA,,,,hapa ninapokwambiya KANUNA HATAKI CHOCHOTE inatakiwa FILIMBI IRUDI...sijuwi itakuwaje,,,watoto aisee...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie sina mtoto lakini nikikumbuka vyenye nilimpa stress mama na baba.. huwa nawafata nawapa pole..tena kuna nengine nawakumbusha wanachekaaaa... inshaAllah nitapata wangu tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe hii mbaya sana. Emu fanyeni ustaarabu
Mm nipo na mwanangu Wa 4.5 yrs ni shida hataki nimguse mama yake

Sasa cku moja nkajua kuwa ameshalala nkaanza kujilia vyangu na Mamake kumbe asimama atuangali mzee niliona aibu sana

Nkaanza kymkomalia alale mwenyw ila kuna wakat anaaigilizia sauti ya kelele za mama yake nkiwa nambandua

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi wa kwangu ni Anamika 2 Sasa huyu mtoto amejua kuhesabu 1..10 kwa kiswahili na kingereza tangu akiwa na mwaka 1.2 na hakuna day care Wala shule yoyote alio enda zaidi ya mama take.

Huyu mtoto mkifika ugenini Basi akitulia zake anaanza kuhesabu ile serious na kwa sauti Hadi watu wanashangaa kwa umri wake imewezekanaje Hadi Kuna siku babu yake akajisifia eti mtoto kachukua akili zake na katika wajukuu ametokea kumpenda haswa.

Alafu pia ni mtoto mwenye maneno ya hekima na kufariji Sana ukimpatia kitu hachoki kusema nashukuru sana,ubarikiwe na Mungu akutunze Sasa kwa umri wake amejizolea umaarufu mtaani atu wanaamini ni malaika maneno yake yanabaraka za kweli hivyo basi wanamnunulia vitu na anapendwa sana.

Kuna siku alilia tumpigie simu Babu yake basi mama yake akafanya hivyo aliishia tu kumuambia Babu yake asalimia Babu , Ashante Babu, Mungu atunze Babu haya maneno Kama umemfanyia vibaya ni maneno yanayo choma Sana.

Kwenye vioja kunasiku badala atumie pot lake kujisaidia yeye akaenda kujisaidia kwenye hotpot Tena hotpot icon ambalo ndio linategemewa kwenye kupamba kabati [emoji1][emoji1][emoji1] hili hotpot lilioshwa lkn Hadi leo halitumiki tunaliogopa .

Akiwa na hasira ni mkali Sana na haijalishi ni Nani atakunyoishea kidole na kukufokea ukitaka aache ni wewe kuondoka Ila ukisema sijui umchape aisee utaua tu bure . Maana anaujasiri mkubwa Sana na misimamo mikali Sana na hayumbishwi kwenye kile anachokiamini .

Pia akiwa katulia anafanya kitu kikiwa hakileti matokeo yale anayo yataka atapandwa na hasira na kuanza kuharibu hicho kitu Kama ni nguo anavaa haivaliki ataibeba kwa hasira na kwenda kuitupa nje [emoji38][emoji38]


NB
Jaman tuwatunze watoto na tuhakikishe ni wasafi wanavutia Sana, mwanao akiwa msafi atapendwa na kila mtu .

Mimi wa kwangu ni star wa mtaa si watu wazima si watoto wenzie wote wanampenda imefika kipindi amewashika masikio Hadi watoto wenzie walio mzidi umri
 
Mwanangu ana miaka miwli kasoro miezi 3
Ni wa kike, anapenda sana kushka simu ya mama hasa ninapokuwa mbali nae

Lengo mama anipigie ili niongee nae

Abi mambo- pwafi,,unacheza- eee,,Sasa muulze kitu ambacho hafanyi mfano
"Unakula mwangu"? Anajbu kwa kutingisha kichwa akimaanisha hapna , kuongea bado taabu kidogo

Juzi nimeingia bandani nikatoa mayai ya kuku mabovu yote,,nikaweka ndani ili mama yake akiamka ayatupe.Nikaenda zangu kazini,saa nne nakuta message ya mama ake mwanao kapasua mayai yote bandani na yale mabovu nyumba nzima inatoa harufu ata hatupiki leo [emoji2][emoji2]

Mama yake anasema huyo mtoto namdekeza sana ngoja anionyeshe yaan ukiamka tu naye yupo tayari daah.
 
Mimi wa kwangu ni Anamika 2 Sasa huyu mtoto amejua kuhesabu 1..10 kwa kiswahili na kingereza tangu akiwa na mwaka 1.2 na hakuna day care Wala shule yoyote alio enda zaidi ya mama take.

Huyu mtoto mkifika ugenini Basi akitulia zake anaanza kuhesabu ile serious na kwa sauti Hadi watu wanashangaa kwa umri wake imewezekanaje Hadi Kuna siku babu yake akajisifia eti mtoto kachukua akili zake na katika wajukuu ametokea kumpenda haswa.
Muombee ulinzi wa Mungu
 
Mi wangu aliona utabiri wa hali ya hewa kwamba mji tuliopo kesho utakuwa na mvua kesho yake ilipofika asubuhi ananiambia mama ule utabiri unadanganya mbona hakuna mvua wakati jana walisema kutakuwa na mvua.

Ikabidi nimwambie mji mkubwa huu hivyo mvua haiwezi kunyesha mji mzima kwa wakati mmoja.
Dogo janja anaendeleaje sasa
 
1.8 anaijua simu ya mama yake na simu zangu na hataki niguse si ya mama ake ama mama yake kugusa simu yangu lah sivyo hua anakua mtata sana mpaka umuamuru akupe kwa rudhaa yake' , anajua ela kuanzia 200 kua ni ndogo na elfu kumi ni kubwa pia anaijua wallet yangu vilivyo na hua nikifika anaichukua na kuihifadhi na ikitokea safari ya dukani ama mama yake anaenda dukani hua anaitoa na kutoa elfu 10 na yeye akijichukulia 500 ama 200 ya coin na akirudi lazima adai change: akiwa macho hataki mtu yeyote kumgusa mama ake hata mm, anajua chombo kichafu na mkimaloza kula yeye ndio hutoa vyombo ikatokea umevigusa hapo ni kazi mpya ya kum'bembeleza" hapendi katuni ni muvee haswa za magari na pikipiki anajua vitu vingi kiasi kwamba namshangaa sana sana tofauti na watoto wengine ninao wa fahamu
That's a very smart kid.
 
Mi wa kwangu balaa natamani akue kidogo labda nitapata zuri la kueleza, leo ni wiki ya tatu sijalala nakesha, dogo analala mchana wakati mimi nipo job, usiku halali na akilala mikononi ukimuweka kitandani tuu yani kabla hata hujakiacha kitanda kishaamka na kelele nyingi, kingine asee usikae karibu na mamaake ugomvi wake c mdogo atalia hapo hadi utashangaa, kingine tangu wiki iliyopita hajacheka sijui ndo kutabasamu hakuna. Ana miezi 4. Hataki kulazwa kama watoto wengine anapokuwa macho, yeye anataka kukaa na anakaa...huyo ni mdogo, kakayake yeye anapenda ngumi, anajua bunduki zote kwa majina, hili nimejaribu kumuonya mamayake asiwe akimuwekea movie za mapigano zaidi ya cartoon lakini sijui huyu kijana anajifunzia wapi maana hakawii kukwambia anataka awe mwanajeshi sababu hapendi majambazi, huyo Ana miaka mi 4, anajua kikorea, kajifunza wapi mi sijui...ila ana shida moja anapenda tambi tuu, vyakula vingine kula mpaka mpigizane kelele sana na husingizia anataka kukojoa akienda harudi..ana huruma sana na mamayake, mjanja mjanja sana ukikasiririka atajua jinsi ya kukufanya ucheke tuu, shida usimuache na mdogo wake peke yao, unaweza kuta mtoto analishwa ugali.
Kama siyo waumini wa dini, huyu wa kukaa macho usiku na kulala mchana mnatakiwa mumubadilishe jina. Anatakiwa kupewa jina la mtu mwingine, especially kama amechukua jina kutoka ukoo wa mama, mnatakiwa mmbadilishe mmpe jina kutoka ukoo wa Baba.

Vinginevyo solution rahisi kabisa kuliko zote, mpelekeni kwa Baba Paroko au kwa Baba Mchungaji
 
Wa kwangu ana miaka 3, kuna siku nimetoka safari nimekaa sebuleni akanifata na kuniuliza "baba leo unalala na mkeo?"
Siku ingine naongea nae kwenye Simu nikamtia mkwara ili ale chakula nae akanambia " baba ntakufumua" Daaaahh nkaona sasa hapa ipo haja ya kununua bunduki mapema.
Ikitokea akaona nimemshika mkono tu mama ake anakasirika sana na kwakua anajua mi haniwezi inabidi aanze kumpiga mama ake ili atoke hapo nilipo (Huyu jamaa anajionaga kama ye ndo ana hati miliki kwa mama ake)
Watoto ni raha sana, wana mambo yao ambayo ni ya kushangaza na kufurahisha kwa pamoja.
[emoji1787][emoji1787][emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787]
 
Huyo ana dalili za wivu kama mwanangu , hata akiwa anacheza bize kiasi gani ukimkumbatia mama yake dogo anakuja mbio mbio anataka mama yake ambebe[emoji23] [emoji23]
Hasa watoto wa kiume[emoji16][emoji16][emoji1787]
 
Back
Top Bottom