Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Mtoto wangu wa 2 ana mwaka sahv ameacha kunyonya tangu akiwa na miezi 7 anapiga msosi bila shida ila ucku njaa ikimshika hata kama ni saa 8 kama hamkubakiza uji kwenye chupa mtapika anashika kitandani uelekeo jikoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto katika hatua zao za ukuaji na kujifunza wanakuwa na mambo flani flani ya kufurahisha sana yaani mwanao anaweza kukuvunja mbavu balaa.
Mfano
1. Mwanangu (1.5years) anaweza kuwa anatazama TV akisikia unaongea na simu au umeweka music kwenye simu anakimbia kuja kuangalia simu hata kama TV ilikuwa na TV program ya katuni nzuri kiasi gani[emoji23] [emoji23] [emoji23]

2. Ukitaka alale we nenda kitandani weka music kwenye simu yako atakuja mwenyewe hata kama alikuwa anakwepa kulala[emoji23]

3. Anaheshimu simu yangu kama kituo cha polisi ila ya mama yake kashaipasua ukiiona utajua mama yake anafanya kazi idara ya miamba (geology)[emoji23]

4.Kupenda safari akiona mtu anatoka tu anaanza kuaga bye bye akijua nayeye anahusika na safari[emoji23] [emoji23]

5. Chakula kikiwa tayari, kabla sijaitwa kula yeye akiona mambo yako tayari anakuja kunipigapiga mgongoni(hajajua kuongea) akiashiria msosi tayari basi ukipotezea anaenda anarudi mpaka utakapoinuka[emoji23] [emoji23]

6. Mwanangu anatabia flani kama wivu, akiona naongea na mama yake mara nimemshika mkono tunaongea kama jambo la siri anakuja fasta analia anataka mama yake ambembe[emoji23]
Nadhani hajajua kwamba mama yake ni mke wangu[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Hivi ni baadi ya vituko vya watoto mdau ongeza vya mwanao
Watoto wanaleta raha sanaaa
Mwisho ndio ume hit

Mimi mtoto wa uncle wangu miaka kama mitano imepita hivi aliniambia kaka we utaoa? Nikamjibu ndio ,Yeye akaniambia tena usitusahau ukioa.Sijui aliwaza nini yule mtoto maana naelekea kuwasahau asee.Sio kwa jalamba hili la Mzee Magu.
 
Nina mdogo wangu ana 3yrs Ke, she'svery smart aisee.. Ukimwita mtoto hataki anasema yeye ni mkubwa (kaanza kuongea ana miezi 8. Kaacha ziwa na waka 1.
Very bold and strong, anakwambia yeye hatakuja kuolewa.
Anaimba Yope yote na kuicheza.
Namkubali alivyo intelligent, nadhani atakua smart kuliko watoto wote nyumbani
Chai maharage hii kaanza kuongea na miezi 8?????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chai maharage hii kaanza kuongea na miezi 8?????

Sent using Jamii Forums mobile app

Wanaongea ila sio maneno yote maneno kadhaa kama mama baba dada acha sitaki, jirani yetu ana mtoto wa kike kwanza kuongea akiwa na miezi8 na kutembelea vitu kafika mwaka anatembea vizuri tu kwenye birthday yake alikua hataki mtu ashike cake yake, anasema acha ya kwanguu
Now ana 1.3+ hivi
 
Mtoto wangu wa 2 ana mwaka sahv ameacha kunyonya tangu akiwa na miezi 7 anapiga msosi bila shida ila ucku njaa ikimshika hata kama ni saa 8 kama hamkubakiza uji kwenye chupa mtapika anashika kitandani uelekeo jikoni

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii tabia yangu kabisa, maana Mama anasema niliacha kunyonya bado mdogo hata mwaka bado usiku kama sikula nikishtuka nadai
 
Wa kwangu ana miezi 9 ana wivu Sana..Kuna mdogo wangu alikuja kunitembelea ana katoto ka miezi 3..kanavutwa kanapigwa kichwani hatari.

Kamejua kuongea neno sitaki..acha toka..Basi kidogo tu achaaa..takiii..popa apa.

Hivi ninavyoandika kana kula chungwa basi kanakula hadi maganda ya nje mara akanyage chungwa lenyewe nampokonya hizo kelele Sasa..hahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi wa kwangu anapenda machungwa. Uji hataki. Ameanza kutambaa, anaenda kila sehemu. Akiona kiti anataka asimame, sema bado hakana balance, mara Pu! Neno lake la trademark ni "aku" sijui kajifunzia wapi. ana miezi 6
 
Mbona hampost tena jamani[emoji5] na corona hii postini basi vioja vya watoto , wengine tupo tu nyumbani, wote watu wazima hamna watoto wadogo[emoji24]

Bby fever[emoji56]
 
1. Wa kwangu ana 1.9 akiwa na kiu anakuja anakushika mkono anakuvuta mpaka kwenye fridge ole wako ukamchukulie maji ya moto pembeni kilio chake kama filimbi, nimegundua mbinu juu ya fridge naweka jagi la maji ya kawaida akinipeleka kwenye fridge nafungua natoa jagi naweka juu ya fridge kenyewe kafupi juu kwa juu na kabadilishia jagi kakinywa sio ya baridi kanasita kama hakajaridhika afu kanakunywa kishingo upande.

2. Kanapenda kuchezea remote ya TV kanatoa betri ole wako urudishe betri unalo hilo mpaka kamepoteza remote kubadili channel tunafanya kubadilishia kwenye kingamuzi.

3. Kamjamaa kana penda kulala karibu na feni ukikasogeza pembeni kanarudi karibtt na feni sasa umeme ukikatika mnalo, kajamaa hakaelewi kitu ni kilio.

3. Kuna baadhi ya matangazo ya biashara kamjamaa kakisikia hata kama kako nje kanacheza katakuja speed kuja kuangalia tangazo likiisha kwa unyongeee kanatoka nje kujumuika na wenzake kucheza.

4. Kajamaa hua kanakua na itikadi za kibabe, kakiona namkumbatia mama yake kanakuja kanamind basi katafanya kila aina ya uayawani wake ilimradi nimuachie mamake.

5. Ukikanunulia pipi (japo nadra sipendelie kumpa ila kanapenda balaa) kakiwa kanalia basi naenda nako dukani kukanunulia, bwanae nunua moja ukisema ununue mbili nyingine utampa badae ye anataka ufungue zote umpe alambe huku kisha huku.

6. Kamjamaa kakivalishwa viatu tu kanajua kuna mtoko, sasa mvalisheni viatu afu muendelee kujichelewesha, kanakufuata kanakushika mkono kanakuvuta mpaka mlangoni afu kanaanza kuguna guna

7. Kajamaa ni kadogo ila kanajua ninapomfokea mama yake kanapoteza furaha mda mwingine kanaenda kujificha chini ya meza haa ha.

8. Kupanda juu ya vitu. Juu ya meza juu ya kinanda changu. Afu akisha panda juu anakojoa aftt anashuka mpaka kamearibu kinanda changu kamekikojolea mpaka kimepata circuit imepiga shoti.

Aise watoto ni faraja sana sana.
 
Back
Top Bottom