Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Hongereni sana wenye watoto...

Napenda sana na ninatamani sana kuwa na mtoto but mda ukifika atakuwepo tena mapacha hahahaa
 
1,2 ni sawa na wa kwangu sasa ana umri wa miaka 3 ila namba nne stori tofauti,simu yangu anaionea kuliko ya mama yake,huyu wangu kila tangazo la tv analolipenda analiiga kama yeye alishiriki kutunga, kiukweli inakuwa faraja sana ukiwa na watoto,stress zako za kutwa zinapozwa na uwepo wao,alhamdulilah
 
Mimi mtoto wa Dada yangu,juzi katoka kutimiza miaka mitano.
Sasa on the date of his birthday mchana wake walikuwa wanacheza,watoto wenyewe kwa wenyewe wakapigana na yeye akashiriki kumpiga mmoja halafu akakimbilia home. Huko nyuma wenzake wakaendelea kupigana mmoja akampiga mwenzie jiwe. Sasa wakasema yeye alikuwepo mama wa mtoto alieumia akaja home anakauliza haka ka my nephew,kakaelezea sasa kakafika hiyo sehemu ambayo na yeye alimpiga mwenzie,akashindwa kusema akaanza kulia kwa nguvu halafu anasema "mama mi Nina usingizi nataka kulala...mi siwezi,kuongea tena Nina usingizi" tukajaribu kumbembeleza akagoma mpaka yule mama akasema basi kaacheni kakalale. Kesho yake Ndio akasema alimpiga lakini kidogo tu sio sana,tulicheka sana. Kana drama Yaani full utundu balaa
Life is very interesting
 
Uzi umenichekesha huu[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Wangu wa kike birthday party yake ya kutimiza two years ndio tulifanya ka party kwasababu angalau mtoto alishaanza kukua tofauti na ile ya 1year, baada ya hapo kwa miaka mitatu mfululizo kila birthday party ya mtu anasema ni yake. Yaani alikuwa anadhani ni yeye tu duniani ndiye mwenye birthday, utasikia birthday yangu, birthday yanguuuuu kilio, hadi mmkalishe na yeye mbele mmvishe na kikofia mmuimbie happy birthday tu yuuuu.... Ndo aridhike la sivyo shughuli nzima ya birthday party itatawaliwa na fujo. Hi hadi shuleni ishawahi tokea kuna zile birthday za watoto wengine zinawakuta wakiwa shule, wazazi wanaenda kufanya kiparty na classmate's yaani alikuwaga analeta fujo hadi naye wamuimbie ndo aridhike. Alienda mbali zaidi na cake anataka iandikwe jina lake hata kama, sio birthday yake, basi hapo itakuwa kilio siku nzima, Akija home kunihadithia utasikia "maa wamechukua birthday yangu... "
Angalau siku hizi amekua anaelewa.

Uyu mdogo wa kiume 3 years jamani mtoto atanitoa jasho huyu anachua bisibisi anachokonoa kila kitu kuanzia vitasa, anasogeza stuli anapanda hadi akifikie kitasa, anachokonoa Tv, akikuta simu kama ni yakufungua utakuta amesambaratisha kila kitu. Kuna siku niliikuta bisibisi kwenye kijibegi chake cha shule jamani jamani.
Mnunuliye vile vi toy vya kuunganisha kuna vya magari vya nyumba n.k. utafanya ubongo uwe creative zaidi ndio ma engineers wanavyo anzaga kutengenezwa una nunua na cd za kufundisha hesabu na vimichiro !!!
 
Kuna mmoja huyo.ccm damu.
Akija mgeni ana muuliza wewee ccm au chadema,
Ukisema chadema .utamsikia afukuza nyumbani kwetu.
 
Hiko kiatu cha mama ake mweee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].....
 
Mi wangu aliona utabiri wa hali ya hewa kwamba mji tuliopo kesho utakuwa na mvua kesho yake ilipofika asubuhi ananiambia mama ule utabiri unadanganya mbona hakuna mvua wakati jana walisema kutakuwa na mvua.

Ikabidi nimwambie mji mkubwa huu hivyo mvua haiwezi kunyesha mji mzima kwa wakati mmoja.
Kumbe una mtoto hongera sana aisee mungu akubarik juu ya hilo.
 
568beded0f7673b0de8b3c5de19e0c55.jpg
568beded0f7673b0de8b3c5de19e0c55.jpg
 
Aisee mie sitaki hata kukumbuka,mwanang alikuwa mtundu balaa at least sasa hivi nimepumua,wakati akiwa na miaka mitano akiwa shuleni (boarding) sijui alitoa wapi mfuko ule wa Salfeti akawachukua watoto wadogo watatu akawafungia kwenye mfuko halaf akawaambia atakayepiga kelele namchapa viboko,akatoka akaenda kucheka bahati nzuri mwalimu akapita pale akaona mfuko unacheza cheza akashangaa kuufungua akakuta watoto walishaanza kuchoka, huku na huku nani kafanya hivi wakamtaja,mwalimu wake ananipigia simu mwanao leo kafanya kosa hili yaani nliishiwa pozi, nkaenda shuleni kwao namuuliza akanambia ahaa niliwaweka watulie maana walikuwa wanasumbua,siku nyingine karudi likizo niko kazini , akaweka Cd tano kwenye radio inayobeba cd tatu, nilivyorudi kanipokea getini akanambia yaani Mom radio yako imegoma kabisaa kuimba leo ahaa itakuwa ulinunua radio ya kichina,nafungua pale kaweka cd kushinda uwezo na sijui alichokonoa nn radio ikafa kabisaaaa
Inabidi pia umuombee mtoto wako hizo traits sio nzuri
 
Mwanangu (5): Baba mbona unapunguza mwendo??
Mimi: Kuna askari mbele
Mwanangu: Sasa usipopunguza mwendo atakufanyaje?
Mimi: Atanikamata
Mwanangu: Akikukamata atakufanyaje?
Mimi: Atanifunga kamba anipeleke gerezani kunifunga.
Mwanangu: Police kazi yake kufunga kamba watu?
Mimi: Ndiyo, ila wale wakorofi tu.
Mwanangu: Hata watoto wadogo anawakamata na kuwafunga?
Mimi: Ndiyo, lakini wale watoto wakorofi wasiopenda kufanya H/W
Mwanangu: Mimi si mkorofi na nafanya HW, si ndiyo baba
Mimi: eeeee mwanangu.
(Tunawakaribia Police wa usalama barabarani tunawapita)
Mwanangu: Police nimewaona watatu pia kuna Mwanamke, baba hata Police Mwanamke yupo
Mimi: Ndiyo
Mwanangu: Na yeye anaweza kukamata watu na kuwafunga?
Mimi: Ndiyo:
(Ukimya dakika 2)

Mwanangu: Baba weka speed One hundred tumeshawapita ma police. (huku akiangalia mshale wa speed-meter)

-------------
Mmmmh uko vzr
 
mie wa kwangu 7,4 yrs huyu mdogo juzi akalilia aombee msosi yeye,akasema tusimame,akaomba MUNGU tusaidie tule vizuri tumalize chakula ,tuoge twende mjini kuogelea(wanapenda sn kuogelea),mwishoni akamalizia pia tukipigana tupigane vzr,hahahahaha,,
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] aaaiii jamani! Nimecheka sana.
 
Mi wa kwangu balaa natamani akue kidogo labda nitapata zuri la kueleza, leo ni wiki ya tatu sijalala nakesha, dogo analala mchana wakati mimi nipo job, usiku halali na akilala mikononi ukimuweka kitandani tuu yani kabla hata hujakiacha kitanda kishaamka na kelele nyingi, kingine asee usikae karibu na mamaake ugomvi wake c mdogo atalia hapo hadi utashangaa, kingine tangu wiki iliyopita hajacheka sijui ndo kutabasamu hakuna. Ana miezi 4. Hataki kulazwa kama watoto wengine anapokuwa macho, yeye anataka kukaa na anakaa...huyo ni mdogo, kakayake yeye anapenda ngumi, anajua bunduki zote kwa majina, hili nimejaribu kumuonya mamayake asiwe akimuwekea movie za mapigano zaidi ya cartoon lakini sijui huyu kijana anajifunzia wapi maana hakawii kukwambia anataka awe mwanajeshi sababu hapendi majambazi, huyo Ana miaka mi 4, anajua kikorea, kajifunza wapi mi sijui...ila ana shida moja anapenda tambi tuu, vyakula vingine kula mpaka mpigizane kelele sana na husingizia anataka kukojoa akienda harudi..ana huruma sana na mamayake, mjanja mjanja sana ukikasiririka atajua jinsi ya kukufanya ucheke tuu, shida usimuache na mdogo wake peke yao, unaweza kuta mtoto analishwa ugali.
Huyo wa miaka minne mcheki DNA ana damu ya kikorea mkuu.......kuanzia lugha mpaka vyakula(tambi) ni vya kikorea
 
Back
Top Bottom