kichongeochuma
JF-Expert Member
- Jan 21, 2024
- 1,669
- 2,864
Nchi hii ifike mahali tuwe na chombo kinacho wasimamia hawa viongozi maana nikama wakisha kuwa na madaraka ya juu basi wapo overall, Haya ya kuendelea kuwaacha waongoze kwa utashi wao na sio kuzongatia sheria kuna siku yatatokea ya Dr. Kleruu na mwamwindi
Mkuu wa mkoa kwa utashi wake anasimama kutangaza kufuta uhamisho wa watumishi wa umma kunyume kabisa na sheria za utumishi wa umma hayo mamlaka anayatoa wapi?
Kwani hakuna sheria zinazo simamia na kuongoza utumishi umma na maswala haya ya uhamisho wa watumishi wa umma ?
Kwamba kwa sasa tanzania ilipo fika ni kwamba utashi wa kiongozi ndio utaamua aendeshe vip eneo lake la utawala na sio kwa mujibu wa sheria?
Tanzania inatatizo sana la kiutawala kiasi kwamba kila kiongozi mwenye mamlaka ya juu anajisikia yeye kuruhusu au kuzuia jambo kwa utashi wake na hakuna mamlaka inayo pinga hii ni kutokana na madhara ya kikatiba na kulindana
Kwa nchi hii ilivyo inawezekana kabisa mkuu wa mkoa akasimama na kutangaza wananchi wote ndani ya mkoa wangu kuanzia kesho mvae kaptula na kukawa hakuna chombo cha kumpinga
Viongozi zingatieni na mfuate sheria kama mnavyo taka mnao waongoza wafuate sheria acheni kuongoza kwa utashi wenu.
Nilitegemea kama kuna vyombo vinavyo simamia hawa watumishi kama vyama vyao vya wafanyakazi vingemrekebisha mkuu wa mkoa manyara na kumwambia bayana asivuke mipaka yake ,ni haki ya mtumishi kuhama na akihamishwa anatakiwa kulipwa kwa mujibu wa sheria na sio utashi
MKUU WA MKOA MANYARA AZUIA UHAMISHO
👇👇👇👇👇👇👇👇👇
www.ippmedia.com