DOKEZO Viongozi kata ya Loya-Uyui -Tabora, watafuna fedha za TASAF

DOKEZO Viongozi kata ya Loya-Uyui -Tabora, watafuna fedha za TASAF

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Joined
Oct 19, 2022
Posts
25
Reaction score
41
Fedha za miradi ya maendeleo za TASAF ndani ya kata Hiyo, viongozi wamegawana wao kwa wao na kuendeleza miradi Binafsi na sio ile ya maendeleo,

Wazee wa kata Hiyo wamepuuzwa na kunyimwa fedha hizo, Mamlaka ya halmashauri inapaswa kufanya uchunguzi wa Jambo hili.

Loya ni mmoja ya kata yenye MAPATO makubwa Sana, kiasi cha million 42 kinakusanywa kwenye kata hii kila mwezi, lakini upigaji umezorotesha maendeleo ya kata hii KILA Mwezi, Hadi leo haina ofisi ya mtendaji wa kijiji, iliyopo ilijengwa KWA tope tangu MWAKA 1968 Hadi leo ni gofu linalotumika kuhidumia wananchi!

Watendaji na viongozi wa CCM kata hii ni wapigaji wanaoshirikiana kuhujumu maendeleo ya kata na wananchi kwa ujumla.

  • Kuna upigaji kwenye ujenzi wa kituo cha zahanati mlimani.
  • Kuna upigaji wa fedha za mikopo iliyotolewa na serikali kwenye halmashauri kuja kata ya loya, viongozi na WATUMISHI baadhi wamegawana na Sasa wanatumia fedha hizo kutengeneza nyavu za samaki.

  • Kuna upigaji wa fedha za kujenga maabara ambazo hadi leo zimetelekezwa na KUWA magofu pale sekondari hakuna juhudi zozote za kuendeleza maabara hizo.
  • Kuna uhujumu wa ukarabati wa Bara Bara ya loya Mabeshi unaofanywa na viongozi wa CHAMA na wafanyabiashara Ili bidhaa zipande Bei!

  • Kuna upigaji wa milion 40 za ujenzi wa Kinga maji la MTO g'hwala ambazo hadi leo hakujajengwa chochote zaidi kulundika mchanga ambao Hadi leo ulishasombwa na maji!!
  • Kata hii inahitaji kikosi kazi KIPYA cha kufuatilia miradi yote ya serikali iliyoletwa kata hii kama ilikamailika na wahusika watapike fedha hizo walizopiga!

Zimenifikia nimezituma kama zilivyo,

Mkurugenzi Uyui anza kazi rasmi, usiwe sehemu ya upigaji huu!
 
Diwani wa CCM kata ya Loya, Katibu Mpya wa CCM Loya na wengineo mnayajua madudu hayo!?

Je nyie kama wawakilishi wa CHAMA mlichukua hatua Gani!?

Au na nyie ni sehemu ya upigaji huu!!?

Makinikeni!
 
Fedha za miradi ya maendeleo za TASAFU ndani ya kata Hiyo,viongozi wamegawana wao kwa wao na kuendeleza miradi Binafsi na sio ile ya maendeleo,
Nimefanya kazi huu mkoa, ile nyie watu mna majungu jamani! Samahani nimesema kiujumla ila sina hakika kama hili uliloleta ni la kweli au la
 
Nimefanya kazi huu mkoa, ile nyie watu mna majungu jamani! Samahani nimesema kiujumla ila sina hakika kama hili uliloleta ni la kweli au la
Mkuu

Unafikiri naleta ya kufikirika!?

Haya nimeletewa na watu wakuaminika,hiyo miradi yote Nenda UONE ni aibu tupu,kwenye maabara kuna milion 60 wakaishia kugonga bati na kutelekeza majengo hadi leo,

TASAFU usiseme wamepiga pesa halafu wanachimba visima vya kienyeji vya futi 15 ambavyo sio thamani ya fedha husika,

Mikopo iliyotolewa wamegawana na muuguzi wa zahanati na Sasa wanatengeneza nyavu za kuvua samaki huko zangeli,vijana na kina Mama ambao ndio walengwa wamepigwa chini KIMYA KIMYA hela zimekopwa na viongozi na WATUMISHI wachache!!

Ni hayo machache mengine ni aibu!!

Pale Loya pale kuna aibu!!
 
Back
Top Bottom