Viongozi kumi (10) Bora Tanzania

Viongozi kumi (10) Bora Tanzania

Tanzania imebahatika kuwa moja ya nchi iliyopata kuwa na viongozi bora kabisa Afrika na hata duniani kwa ujumla.Viongozi hao wamepata kuwa na mchango mkubwa Tanzania na hata kwa bara la Africa. Tunaona mifano ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye amepigania uhuru si kwa nchi ya Tanzania tu bali amekuwa na mchango mkubwa katika harakati za uhuru kwa nchi jirani kama Afrika Kusini, Zambia na Msumbiji.

Tanzania pia imepata kuwa na wanaharakati na wapigania uhuru mahiri walioweza kuitwaa nchi kutoka katika kucha za wakoloni. Tunaona wapigania uhuru na wanaharakati kama Kinjekitile Ngwale, Bwana Abushiri na Bibi Titi Mohammed. Viongozi kama Mtemi Isike, Chifu Mirambo, Mangi Meli na wengineo wengi ambao walikuwa viongozi wa kimila walikuwa mstari wa mbele katika mapambano ya uhuru na hatimaye kuikomboa na kutupatia Tanzania hii tunayoifurahia leo.

Bila kupoteza muda, Naomba niweke orodha fupi ya viongozi waliopata kuongoza Tanzania walioacha alama kubwa na historia ya kipekee kwa ubora wao na uwezo wao wa kiuongozi ambao pasi na shaka uliacha alama kubwa kwa watanzania.

Kwa sasa nitaweka orodha tu kwa kifupi ila nitarejea kuelezea kila mmoja kwa undani zaidi.Pamoja na kuongeza orodha mpaka kufikia kumi (10) Bora.

Updates; Moderators naomba mnibadilishie Title iwe Kumi (10) Bora badala ya Tatu (3) Bora. Ahsante

Viongozi Kumi (10) bora kuwahi kuwepo Tanzania.

1. Mwl.Julius Kambarage Nyerere (Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)
View attachment 1752017

2. Edward Moringe Sokoine ( Waziri Mkuu wa Tanzania 1977–1980 na 1983 - 1984)
View attachment 1752018

3. John Pombe Magufuli (Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)
View attachment 1752024

4. Chief Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga (Mkwawa) - Chifu wa kabila la Wahehe
View attachment 1752828


5. Benjamin William Mkapa (Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)

View attachment 1752030


6. Rashidi Mfaume Kawawa ( "Simba wa Vita" - Waziri mkuu wa Tanzania 1972 - 1977" )

View attachment 1752641


7.Ali Hassan Mwinyi ( Rais wa Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1985 - 1995 )

View attachment 1752648


8.Oscar Salathiel Kambona ( Waziri wa Mambo ya Nje 1963–1966 )

View attachment 1753512

9. Jakaya Mrisho Kikwete ( Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2005 - 2015)

View attachment 1753513

10. Abeid Amani Karume ( Rais wa kwanza wa Zanzibar 1964 - 1972 )

View attachment 1753522
Toa yule muuaji wa tatu! tupa kule! asituharibie hii list. Weka Aboud Jumbe afadhali
 
Back
Top Bottom