Viongozi Simba bado wanaingilia bench la ufundi?

Viongozi Simba bado wanaingilia bench la ufundi?

Nakubaliana na wewe Tshabalala na Gadiel wanafanana kila kitu, kwa mechi kubwa hawa wanatakiwa waanzie benchi. Tshabalala anaongoza kwa kujifunga mwenyewe
mi nahisi wanaingilia hata upangaji Fraga hata kwenye benchi hayupo shibob pia hayupo waliowataka wamevurunda wanashindwa kufanya sub shabalala timu ya taifa anawekwa benchi na Gadiel Michael lakini huku ndio ana namba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sesten Zakazaka,

Klabu za Tanzania ikiwemo na Simba hakuna Kocha ambae ni Manager kwenye benchi la Ufundi Bali kuna Head Coach.
Ukisema Simba ina sajiri bila kufata matakwa ya benchi la Ufundi ni wazi haufahamu kuhusu majukumu ya Head Coach.
Kocha ambae ni Manager kwenye timu ni msimamizi na mwajiri wa benchi zima la Ufundi sambamba na wachezaji..Pia ni msimamizi wa mambo yote ya Ufundi ikiwemo mfumo wa kucheza,falsafa ya timu na aina ya wachezaji watakao tumika kwenye mchezo.Aidha ana husika moja kwa moja kwenye soko la usajiri.

Head Coach ni msimamizi wa mambo yote ya Ufundi ndani ya uwanja.Hana mamlaka ya kuajiri bali ana toa mapendekezo tu ya nani asajiriwe.

Sasa kutoa lawama kwa Simba kufanya usajiri ni kuwakosea heshima Simba,kwa maana wako sahihi kabisa.
Simba kocha wake sio Manager bali ni Head Coach...kwa maana hiyo baada ya msimu kumalizika,Head Coach ana andika ripoti yake ya msimu mzima.

Ripoti hiyo ina kuwa na mambo mengi ikiwemo mapendekezo ya wachezaji gani wasajiriwe na wachezaji gani waachwe.
Kumbuka hayo ni mapendekezo sio maamuzi ya mwisho...!!! Mapendekezo hayo yana pitiwa na kamati ya usajiri kisha kamati ya usajiri ina Fanya upembuzi wa usahihi wa ripoti hiyo.

Kamati ina sajiri kulingana na bajeti yao ya msimu na nini malengo yao kama timu.

Ulaya timu nyingi zina mfumo wa kocha kuwa Manager hivyo ana pewa fungu la usajiri,huku akisimamiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu.

Klabu za Tanzania hazina cheo cha mkurugenzi wa Ufundi bali wana kamati za mashindano na kamati za usajiri...hizi ndizo zenye maamuzi ya mwisho kuhusu usajiri...baada ya kupitia ripoti ya kocha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe nae mbumbumbu hamna kitu.
Umesema head coach anatoa mapendekezo nani asajiliwe ..

Sasa kwanini hiyo kamati ya usajili isilete hao wachezaji ambao head coach kawataka kwenye ripoti yake?? Nini kinashindikana?

Hiyo kamati unayosema IPO sahihi, inawezaje kuleta wachezaji tofauti na ambao kocha anawataka?. Ukizingatia wale ambao head coach kapendekeza wasajiliwe, anakuwa kashapanga atawatumia vipi na watafit kwenye formation zake..!

Iweje aletewe mchezaji ambaye hajui hata aanze kumtumia vipi??
 
Wewe nae mbumbumbu hamna kitu.
Umesema head coach anatoa mapendekezo nani asajiliwe ..

Sasa kwanini hiyo kamati ya usajili isilete hao wachezaji ambao head coach kawataka kwenye ripoti yake?? Nini kinashindikana?

Hiyo kamati unayosema IPO sahihi, inawezaje kuleta wachezaji tofauti na ambao kocha anawataka?. Ukizingatia wale ambao head coach kapendekeza wasajiliwe, anakuwa kashapanga atawatumia vipi na watafit kwenye formation zake..!

Iweje aletewe mchezaji ambaye hajui hata aanze kumtumia vipi??
Upo sahihi kabisa mkuu
 
Hautakiwi kuilaumu Simba pekee...huu ndio mfumo mzima wa Soka letu hata Yanga wana hizi kamati...nenda Mtibwa,Azam Fc.
Alafu sijakubaliana na hoja yako...nimekujibu kwa Fact.
Manchester United hawa mkurugenzi wa Ufundi wana mtu ambae hajuhi mpira Ed woord..huyu ni kama Hans Pope unae msema Simba Je wana mafanikio gani?
Una tambua kama kwamba klabu nyingi tu za ulaya kocha afanyi usajiri?


Sent using Jamii Forums mobile app
acha uongo..

Mfumo wa uendeshaji soka ulaya na huku ni tofauti..
Ulaya hamna head coach, huyo head coach anatambulika Kama team manager na ndo bosi wa wachezaji..

Halafu Ed ni bosi mtendaji wa team, ina maana yeye ni kiunganishi kati ya wachezaji na kocha (manager) na bodi kuu ya watendaji including wanahisa na matajiri wa team...
Pia ni kweli man u hawana mkurugenzi wa ufundi that's why ed anasimama Kama mkurugenzi wa ufundi.. Lakini sio kazi yake.
Kazi yake ni kufutatilia utendaji wa kila siku wa club then kupeleka juu kwa mabosi..

Ulaya suala la usajili ni manager (kocha) ndo anapendekeza then mkurugenzi wa ufundi anatuma scouts waende kumuangalia mchezaji husika, walete taarifa. Kisha kina Ed wao wanapeleka taarifa kwa bodi ya juu wapewe pesa ya usajili. Kazi ya kumleta mchezaji inabaki kwa mkurugenzi wa ufundi.

Sasa utafanishaje na bongo kwenye ujanja ujanja??
 
Usikariri kaka kuhusu upigaji kwenye klabu.
Yanga kulikuwa na kikundi kinaitwa Yanga Family hawa walikuwa wana Fanya usajili wa timu.Hawa ndio una waitwa wapigaji wakati wewe hata shilingi mia hautoi,unajua kulaumu tu.Simba kulikuwa na Friends Of Simba...ndio hao wakina Hans Pope ambae wewe una sema wapigaji...hawa ni watu wenye pesa zao.
Kuendesha soka ni kazi kubwa sana.
Kuhusu ripoti nimekwambia imebeba mambo mengi sana,hivyo kwenye kamati ya Ufundi kuna undwa na watu wenye utaalamu tofauti tofauti.Mfano Yanga Mshindo Msolla ni Kocha kitaaluma pia ni Dr wa mifungo..Simba Mwina Seif Kaduguda ni Kocha na mwandishi wa habari kitaaluma...sasa hawa watu wana uwezo mkubwa kwenye nyanja hiyo.
Kwa kukusaidia mfumo wa kamati kusajiri hauko Tanzania tu hata nchi nyingi za Afrika kaskazini kama Misri na nyinginezo wana tumia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao yanga family na friends of simba walikuwa hawasajiri bali wanatoa pesa kwa ajili ya usajili..

Sasa Wewe unadhani et wao wanaenda moja kwa moja kuleta mchezaji wao wanampa kocha..! 😁😁😁

Wao wanapewa mapendekezo na kocha nani achukuliwe wao wana play kama sponsor's...

Huu mfumo upo bongo tu ulaya kila mtu ana kazi yake huwezi kuwa na professional mbili ndani ya team, lazima ushindwe kufanya kwa ufasaha..

Yanga na simba kwa ukubwa wote ule mpaka leo zinashindwa kujiendesha zenyewe..! What a joke
 
Simba inatia mashaka sana. Ni kama timu iliyokosa mbinu. Tusidanganyane tulikua na hamu na shauku kubwa ya kubeba kombe la Mapinduzi ndio maana tulapeleka kikosi kamili Zanzibar. Wachezaji, benchi la ufundi na hata viongozi wa timu wanatuangusha

Hoja yangu ni ileile tumesajili vibaya kuanzia wachezaji hadi kocha! Na hili ni kosa na dosari ya moja kwa moja ya viongozi wa club yetu. MO anapigwa pesa nasema, aamke
 
Hivi ni kocha gani aliyemsajili Gadiel na Ajibu wakati akijua kabisa kuwa namba hizo zina wachezaji wengi au ilikuwa kumkomoa Yanga haiwezekani wachezaji wa timu ya Taifa kusugua benchi Simba bali wao waliyataka mpira ndio unaisha hivyo Gadiel na Ajibu rudini Yanga hao Simba wanasajili tu kila wanayemwona matokeo yake ni kusugua benchi na timu ya Taifa huwezi kuitwa
 
Kwenye usajili wa dirisha kubwa Simba ilitakiwa iongeze wachezaji watatu tu mshambuliaji mmoja asili mwenye uwezo sawa na Kagere au zaidi yake, kiungo mkabaji mkata umeme mwenye roho mbaya mwenye uwezo wa hali ya juu wa kupora mipira na kipa mahiri. Matokeo yake ikapoteza sehemu ya uti wa mgongo wa timu kwa kuondoka Okwi, Kotei, Gyan na Niyozima halafu wakaletwa wabrazili. Sasa leo wanatafutana uchawi wakati wamejiloga wenyewe. Ila ndio Simba ndio zao waliwahi kumuacha Hamis Tambwe akiwa anaongoza ufungaji bora halafu wakamsajili Nserekuma.
 
Kwenye usajili wa dirisha kubwa Simba ilitakiwa iongeze wachezaji watatu tu mshambuliaji mmoja asili mwenye uwezo sawa na Kagere au zaidi yake, kiungo mkabaji mkata umeme mwenye roho mbaya mwenye uwezo wa hali ya juu wa kupora mipira na kipa mahiri. Matokeo yake ikapoteza sehemu ya uti wa mgongo wa timu kwa kuondoka Okwi, Kotei, Gyan na Niyozima halafu wakaletwa wabrazili. Sasa leo wanatafutana uchawi wakati wamejiloga wenyewe. Ila ndio Simba ndio zao waliwahi kumuacha Hamis Tambwe akiwa anaongoza ufungaji bora halafu wakamsajili Nserekuma.
Nakubaliana na MO kua kuna watu pale Simba wana interest zao na wala hawako pale kwa ajili ya club
 
Back
Top Bottom