Sesten Zakazaka,
Klabu za Tanzania ikiwemo na Simba hakuna Kocha ambae ni Manager kwenye benchi la Ufundi Bali kuna Head Coach.
Ukisema Simba ina sajiri bila kufata matakwa ya benchi la Ufundi ni wazi haufahamu kuhusu majukumu ya Head Coach.
Kocha ambae ni Manager kwenye timu ni msimamizi na mwajiri wa benchi zima la Ufundi sambamba na wachezaji..Pia ni msimamizi wa mambo yote ya Ufundi ikiwemo mfumo wa kucheza,falsafa ya timu na aina ya wachezaji watakao tumika kwenye mchezo.Aidha ana husika moja kwa moja kwenye soko la usajiri.
Head Coach ni msimamizi wa mambo yote ya Ufundi ndani ya uwanja.Hana mamlaka ya kuajiri bali ana toa mapendekezo tu ya nani asajiriwe.
Sasa kutoa lawama kwa Simba kufanya usajiri ni kuwakosea heshima Simba,kwa maana wako sahihi kabisa.
Simba kocha wake sio Manager bali ni Head Coach...kwa maana hiyo baada ya msimu kumalizika,Head Coach ana andika ripoti yake ya msimu mzima.
Ripoti hiyo ina kuwa na mambo mengi ikiwemo mapendekezo ya wachezaji gani wasajiriwe na wachezaji gani waachwe.
Kumbuka hayo ni mapendekezo sio maamuzi ya mwisho...!!! Mapendekezo hayo yana pitiwa na kamati ya usajiri kisha kamati ya usajiri ina Fanya upembuzi wa usahihi wa ripoti hiyo.
Kamati ina sajiri kulingana na bajeti yao ya msimu na nini malengo yao kama timu.
Ulaya timu nyingi zina mfumo wa kocha kuwa Manager hivyo ana pewa fungu la usajiri,huku akisimamiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu.
Klabu za Tanzania hazina cheo cha mkurugenzi wa Ufundi bali wana kamati za mashindano na kamati za usajiri...hizi ndizo zenye maamuzi ya mwisho kuhusu usajiri...baada ya kupitia ripoti ya kocha.
Sent using
Jamii Forums mobile app