Viongozi Simba bado wanaingilia bench la ufundi?

Viongozi Simba bado wanaingilia bench la ufundi?

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
Sizungumzii matokeo ya juzi kati ya Simba na mtani wetu Yanga bali hizi ni lawama za muda mrefu kwamba kocha mkuu hua anaingiliwa majukumu yake, kwanza ya kuchagua wachezaji wanaosajiliwa na pili hata kupanga timu kwenye baadhi ya mechi.

Malalamiko ya Patrick Aussen kuhusu jambo hilo sio ya kwanza lakini angalau yeye alijitokeza wazi kusema. Kuna baadhi ya wachezaji kama James Kotei hakutaka waondoke na wengine kama Mbrazil aliyevunjiwa mkataba yeye kama mwalimu hakushirikishwa kwenye kumsajili.

Nina wasiwasi hata huyu jamaa kutoka UD Songo hakua pendekezo la mwalimu Sven kwa sasa bali ni katika kulekule kukurupuka na kupiga dili kwa viongozi wa Simba kusajili wachezaji tofauti na mahitaji ya timu tena pengine kwa vile tu waliisumbua Simba pale ilipokutana na timu zao.

Mapungufu kwa Simba yapo kwa strikers, tena orthodox stickers, wale wanaojua kumalizia na wanaojua nyavu na nyavu zinawajua kama Kagere. Sijui ni kiasi gani Simba walilazimika kulipa ili kuvunja mkataba na yule Mbrazil lakini ni kweli walishindwa kupata mtu kama Makambo?

Kuna harufu ya ufisadi kwenye usajili. Haohao kina Manara na viongozi wengine wa Simba wanafaidika na pesa za Mo kwa namna moja au nyingine wanapofanya usajili na Board isiposhtuka mapema Simba SC itabakia kua timu iliyotumia pesa nyingi kwenye kusajili Tanzania lakini inajaza wachezaji wasiotumika wala kuhitajiwa kwenye timu
 
Ngoja waje
Najua watakupinga sana
 
Huyu anakuja kukaa benchi au kumyima namba kiungo mwingine wa nje, na akifit na mfumo basi kuna proo mwingine wa kukatw, Shangaa kukataa kumuongezea ela Kotei na kurudia rudia yaleyale
Huo ni ujuaji na ujanjaujanja wa viongozi wa Club yetu
 
Sesten Zakazaka,

Klabu za Tanzania ikiwemo na Simba hakuna Kocha ambae ni Manager kwenye benchi la Ufundi Bali kuna Head Coach.
Ukisema Simba ina sajiri bila kufata matakwa ya benchi la Ufundi ni wazi haufahamu kuhusu majukumu ya Head Coach.
Kocha ambae ni Manager kwenye timu ni msimamizi na mwajiri wa benchi zima la Ufundi sambamba na wachezaji..Pia ni msimamizi wa mambo yote ya Ufundi ikiwemo mfumo wa kucheza,falsafa ya timu na aina ya wachezaji watakao tumika kwenye mchezo.Aidha ana husika moja kwa moja kwenye soko la usajiri.

Head Coach ni msimamizi wa mambo yote ya Ufundi ndani ya uwanja.Hana mamlaka ya kuajiri bali ana toa mapendekezo tu ya nani asajiriwe.

Sasa kutoa lawama kwa Simba kufanya usajiri ni kuwakosea heshima Simba,kwa maana wako sahihi kabisa.
Simba kocha wake sio Manager bali ni Head Coach...kwa maana hiyo baada ya msimu kumalizika,Head Coach ana andika ripoti yake ya msimu mzima.

Ripoti hiyo ina kuwa na mambo mengi ikiwemo mapendekezo ya wachezaji gani wasajiriwe na wachezaji gani waachwe.
Kumbuka hayo ni mapendekezo sio maamuzi ya mwisho...!!! Mapendekezo hayo yana pitiwa na kamati ya usajiri kisha kamati ya usajiri ina Fanya upembuzi wa usahihi wa ripoti hiyo.

Kamati ina sajiri kulingana na bajeti yao ya msimu na nini malengo yao kama timu.

Ulaya timu nyingi zina mfumo wa kocha kuwa Manager hivyo ana pewa fungu la usajiri,huku akisimamiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu.

Klabu za Tanzania hazina cheo cha mkurugenzi wa Ufundi bali wana kamati za mashindano na kamati za usajiri...hizi ndizo zenye maamuzi ya mwisho kuhusu usajiri...baada ya kupitia ripoti ya kocha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tambala mbovu,

Naona unakubaliana na hoja yangu kwa namna ingine.Huoni kama huo mfumo ndio unaolea tatizo la kusajili wachezaji wasio na uwezo? Kwasababu unatoa mianya kwa watu wasio na ujuzi kuingilia kazi za kocha

Simba kwa mfano kamati ya usajili yupo mtu kama Zakaria Hanspop!!! Hana ajualo kuhusu mifumo n falsafa ya timu wala mbinu zozote za ndani ya uwanja. Sasa atawezaje kuitafsiri ripoti ya mwalimu kuhusu mahitaji ya kiufundi ya timu ikiwemo aina ya wachezaji hata kama kapelekewa kwenye ripoti ya kocha? Wanachofanya wanahudhuria mechi za Simba na wakiona mchezaji anawasumbua kwa chenga basi wanafanya mazungumzo na timu yake au yeye mwenyewe na kisha wanamsajili na kumpelekea mwalimu

Utaratibu huu kwanza unatoa mianya ya kufanya ufisadi maana kwanza hauna checks and balances. Mwalimu anapotoa pendekezo kwamba mchezaji fulani asiuzwe au asitolewe chakushangaza inakaa kamati ya ma layman na kuamua aondoke! Sasa timu ikiwa na pengo kwenye nafasi hiyo mtamlaumu kocha?
 
Huyu anakuja kukaa benchi au kumyima namba kiungo mwingine wa nje, na akifit na mfumo basi kuna proo mwingine wa kukatw, Shangaa kukataa kumuongezea ela Kotei na kurudia rudia yaleyale
Mie Kotei nilikuwa simkubali pale ambapo katika pasi kumi anazopiga mbili tu ndo zinaenda kwa mchezaji mwenzake. Uliza kama anapata namba huko aliko kabla hujalalamika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie Kotei nilikuwa simkubali pale ambapo katika pasi kumi anazopiga mbili tu ndo zinaenda kwa mchezaji mwenzake. Uliza kama anapata namba huko aliko kabla hujalalamika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Very reasonable argument.Lakini kumbuka Kotei basically ni mkata umeme, inawezekana hakua na vitu viingi sana uwanjani ila alikua hafanyi makosa kama lile la Mzamiru la kumuachia Balama achukue mpira kirahisi na apige shuti lililozaa goli

Ni kweli pia huko alikokwenda hana uhakika wa namba, lakini yote inategemea na mifumo na aina ya wachezaji aliowakuta na aina ya ligi na ushindani, ila kwa Simba alikua anahitajika na mwalimu alilisema wazi
 
Hata huko ulaya kwenye mameneja kuna usajili wa hovyo wakati mwingine, kama Arsenal, kwa sababu mbalimbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nikweli hata Ulaya nako sometimes kuna usajili wa hovyo lakini ni mara chache kama ambavyo wakati fulani vilabu kama Real Madrid na AC Milan vilikua vinataka kua na wachezaji wote bora duniani na usajili ukawa unafanywa na Marais wa vilabu hivyo!

Lakini kwa kawaida wanaosajili ni watu wa ufundi "tactician" na hata ikitokea makosa inakua ni bahati mbaya kutokana na ku overlook lakini sisi makosa yetu yanakua na "hila" ndani yake, kunakua na dhamira ovu ya upigaji kwenye usajili sometimes
 
Wakati kocha anasalimiana naye picha wakati wa utambulisho,kishingo alikuwa anamshangaa mchezaji maana hajawahi kumuona na mchezaji anamshangaa kocha.

Mikia acha waitwe mikia tu
Nina hakika kama kocha angepewa nafasi ya kumuona akicheza au kumfanyia majaribio Mmozambique angekua na opinion nyingine kufuatana na mahitaji ya kiufundi ya timu, mfumo autakao, uwezo au mapungufu ya wanaocheza nafasi hiyo na pengine hata umbile tu na kimo cha mchezaji mwenyewe
 
Nina hakika kama kocha angepewa nafasi ya kumuona akicheza au kumfanyia majaribio Mmozambique angekua na opinion nyingine kufuatana na mahitaji ya kiufundi ya timu, mfumo autakao, uwezo au mapungufu ya wanaocheza nafasi hiyo na pengine hata umbile tu na kimo cha mchezaji mwenyewe
Wamejaza wachezaji wa aina moja kibao..........ndiyo maana timu haina plan B
 
Back
Top Bottom