Kuna mafala wa upande wa pili wamegawana majukumu, kuna kundi moja liko Mafia, Morogoro na Zanzibar kuiharibia Simba jumapili ili wao jmosi wakipita watucheke na mji tuuone mchungu.
Kundi la kwanza ni lao wenyewe linalopambana kuhakikisha kesho wanafuzu baada ya miaka kibao kuishia njiani na kweli wamechafua sana mazingira kwa ajili ya mchezo wa kesho.
Viongozi wa Simba, saa hizi ni mbaya, kufuru lifanyike hata kama kunitoa kafara mie ili jumapili tufuzu niko tayari, chonde chonde Viongozi, mji tunautaka huu kuendelea kuishi, hawa malofa wanafanya haya mambo kimya kimya, wanakuja had kwenye mazoezi yetu wanaokota mchanga na nyasi wanazipeleka kwa wataalamu wao ambao wamehifadhiwa Chanika.
Tusimuamini mtu, msiwaone wanaongelea yao, Leo nimewaona baadhi ya wachezaji na Viongozi wao wakiipelekwa Chanika kupewa 'vijiti' vya kutumaliza kesho, tusipojihadhari wanaweza kutupiga bao 1 0 au 2 1.
Mjumbe hauawahi, kama nadanganya au natafuta Kiki sawa lakini chukueni tahadhani, tunataka furaha t jumapili.