Viongozi wa Afrika Mashariki kukutana leo kujadili mzozo wa DRC, Rwanda

Viongozi wa Afrika Mashariki kukutana leo kujadili mzozo wa DRC, Rwanda

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
1655706820614.png

Viongozi 7 wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatarajiwa kukutana leo Juni 20, 2022 Jijini Nairobi, Kenya mada kuu ikiwa ni mgogoro unaoendelea kati ya DRC na Rwanda.

Kumekuwa na mapigano makali yanayofufua uhasama wa miongo kadhaa kati ya mataifa hayo mawili, ambapo DRC inailaumu Rwanda kwa kusapoti kundi la waasi la M23, lakini Rwanda imekuwa ikikanusha madai hayo.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alitoa wito wa kutumwa kikosi cha kikanda ili kurejesha amani, lakini DRC ilikataa kukubali ushiriki wa Rwanda katika operesheni hiyo.

===

East Africa leaders to meet Monday to discuss DR Congo conflict

The leaders of seven nations comprising the East African Community bloc will meet Monday to discuss the security situation in the Democratic Republic of Congo's violence-torn east, the Kenyan presidency said.

The meeting comes as heavy fighting revives decades-old animosities between Kinshasa and Kigali, with the DRC blaming neighbouring Rwanda for the recent resurgence of the M23 rebel group.

Rwanda has repeatedly denied backing the rebels while both countries have accused each other of carrying out cross-border shelling.

Source: Bangkokpost
 
Wachukue hatua kali kwa huyo mvamizi, hata kumsimamisha uanachama ikibidi.
 
Mazungumzo yameshashindwa hata kabla ya kuanza. M7 na PAKA ndio wanaofadhili M23 then mnajadili nini? Labda SADC lakini nani atabeba hizo gharama?
 
Hivi Rwanda aliwezaje kusaidia kupambana na wale wa Msumbiji ambao hana ukalibu nao, anashindwa kupambana M23 ambao wanamsumbua jirani yake.
Msemaji wa Jeshi la Congo amesema Jeshi la Congo Ni Jeshi la 8 kwa nguvu Africa,so acha wapambane na M23.
 
Back
Top Bottom