Viongozi wa CCM na Serikali mnajisikiaje mkiuona uwanja wa Azam Complex?

Viongozi wa CCM na Serikali mnajisikiaje mkiuona uwanja wa Azam Complex?

Mbuzi mee

Senior Member
Joined
Dec 29, 2022
Posts
156
Reaction score
217
Yaan ina tia hasira na pia inahuzinisha, mnashindwa ingia ubia na wamiliki wa Ccm wanaomiliki viwanja vingi mapato yakaenda halmashauri kwenye mgawanyo? hao waarabu wanaotunyanyasa ubora wa viwanja vyao unachangia.

Huku mnaweza fanya kitu kizur kikatutambulisha watanzania. Hata mashindano yenu ya serikali ya wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo yakifanyika kwenye viwanja hiv kimkoa au kitaifa vikifanyika vitaongeza hamasa kwa vijana na kuvutiwa zaid na mpira na badae tutakuja jenga timu bora sana

Kwa leo ni hayo tu…
 
Tuache kuunda mifumo tukajinunulie lc300 tuanze kujenga viwanja acha ujinga mpira wa bongo bado ni maneno mengi akili zikiwakaa sawa tutafikiria kujenga viwanja bora acha tukimbizane na lc na watoto wetu wakasome pazuri
 
Yanagimbania mapato tu majizi makubwa. Viwanja virudishiwe halmashauri, zivikodishe kwa wawekezaji period. Sisiem ni majambazi Mbuzi
 
Yanagimbania mapato tu majizi makubwa. Viwanja virudishiwe halmashauri, zivikodishe kwa wawekezaji period. Sisiem ni majambazi Mbuzi
Huwa naamin Congo pasingekuwa na ma vita yao..pangekuwa na viwanja bora sana na hata kombe la mataifa ya Afrika yangekuwa tayari hata yameshafanyika..

Yaan ukiangalia nchi zilizotuzunguka kimpira sisi mazingira yana tupendelea sana kuwa bora na kuwavutia waje kucheza hapa...
 
Ni aibu mkuu ila wao hawajari,viwanja vingeboreshwa hata vijana wengi wangejitoa na kuona umuhimu wa kucheza soka la kulipwa
 
Huwa naamin Congo pasingekuwa na ma vita yao..pangekuwa na viwanja bora sana na hata kombe la mataifa ya Afrika yangekuwa tayari hata yameshafanyika..

Yaan ukiangalia nchi zilizotuzunguka kimpira sisi mazingira yana tupendelea sana kuwa bora na kuwavutia waje kucheza hapa...
Mbuzi uko sahihi sana. Ule msemo wa penye miti hapana wajenzi siupendi kabisa, umekaa kinafiki sana
 
Viwanja vingi vya michezo nchini ni mali ya Watanzania! Ni kwa bahati mbaya sana ccm wamevikwapua kinyemela.

InshaAllah ipo siku atatokea Kiongozi Mzalendo, na atakubaliana na wadau wa michezo kuviweka chini ya usimamizi wa Halmashauri zetu.
 
Na iwe hivyo amiina vipewe halmashaur kuwajibika kuvitunza..
halmashauri itakayoshindwa kuvitunza viongoz wake watatakiwa kuwajibishwa...
 
Hela yote ya viwanja vya mpira inaenda kwenye account ya ccm mkoa kwa ajili ya kuwapa askari wetu wanaosimamia uchaguzi wa chama.
 
Back
Top Bottom