Viongozi wa CHADEMA msitafute huruma ya wananchi kupitia kiki za matukio, mtaumia bure

Viongozi wa CHADEMA msitafute huruma ya wananchi kupitia kiki za matukio, mtaumia bure

Mr Tyang

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2018
Posts
1,727
Reaction score
6,807
Wanabodi Natumai mpo salama na Mungu anaendelea kutuepusha na hili janga la Covid19 Basi naomba niende kwenye mada bila kupoteza muda.

Leo asubuhi nimekutana na habari ya kuvamiwa
kwa mwenyekitii wa Chadema, Mh freeman Mbowe akiwa Dodoma.
Hivyo ikabidi nifuatilie undani wa taarifa zaidi, nanukuu nilichokisikia kutoka kwa Tumain makene Kupitia sauti ya simu;

"Nikweli mwenyekiti wetu amevamiwa na kundi la watu wasiojulikana mida ya sa6-7 usiku wakati akirejea nyumbani kwake, kundi Hilo lilimuvizia alipokuwa akipanda ngazi za kuelekea nyumban kwake Dodoma na likampiga na kumjeruhi. Amekimbizwa hospital kwa ajili ya matibabu zaidi taarifa zaidi tutazitoa baadae" Tumain Makene Msemaji wa idara ya nawasiliano Chadema.

Kwamaelezo hayo yamenifanya nipate ukakasi juu ya hilo tukio na kufanya nilione kwa asilimia kubwa Kama Ni kiki za kisiasa tu za kujarbu kutafta huruma kwa wananchi. Miongoni mwa masawali yanayotatiza juu ya hilo tukio Ni hayapa;

1. Je Mh Mbowe Hakuwa na walinzi/Wapambe Tena mida ya usiku Kama Ile? Na Kama alikuwa nao mbona wao hawajaripotiwa kukwaruzwa Wala kupambana na hao wavamiaji?

2. Wavamizi waliingiaingia je ndani ya eneo la nyumba ya Mbowe mpaka wakamusubiri apaki gari lake akaanza kupanda ngazi ndo wakamuvamia? Nikweli nyumba ya kiongozi mkubwa Kama Mbowe haina walinzi kweli Hadi watu waingie kirahisi vile? Na Kama wapo walipambana na hao wavamizi?

3. Nikweli Mbowe pale dodoma anaishi mwenyewe tu Hakuna mtu mwingine anaeishi nae? Na Kama yupo je mbona yeye hakuumizwa Wala kujeruhiwa au hao wavamizi walikuwa ghosts?

4. Nikweli tukio la Mbowe limekaa kisaiasa au kijamii , ikumbukwe pia Wabunge wetu huwa wanatabia ya kuingilia mahusiano ya watu wanapokuwa huko bungeni(hili lipo wazi) japo simanishi ndo Sababu ila inaweza wekwa kwenye kudhani pia.

NOTE; Ikumbukwe tukio hili la uvamizi halijafanyika barabarani,bar,ofisini na n.k Bali limefanyika eneo la makazi ya Mbowe Tena akipanda ngazi.

#Viongozi punguzeni kiki za kisiasa mtakuja kuumia halfu bila kupata hiyo huruma mnayoitafta.
#Watu punguzeni kudhurula usiku wa manane pia. Mpaka inafika sa6+ hujarejea nyumbani tu huo Ni udhurulaji hata Sheria ya udhurulaji ipo wazi juu ya hili. Pia tusisahau kuwa usiku una Mambo mengi sana.

Ahsanteni.
 
"Hakuwa na walinzi maana waliondolewa kipindi cha sakata la Corona, sasa wakati anapanda ngazi wakashuka watu watatu wakamuambia wewe unaisumbua sana Serikali, sisi hatuna mpango wa kukuua ila tunataka tukuvunje ili ushindwe kufanya kampeni" - Msigwa Peter
 
Hawa wameshaigeuza iyo ya kuvamiwa ndo sera, wananchi tumeshituka, atakaye wapa kura hakika ana maslai ya moja kwa moja nao lasihivyo hawapati kitu hapa
 
Kwani kuna tukio lolote walilofanyiwa upinzani na serikal ikakemea hilo?
 
Unakuta aliyeandika bado hata hajapiga mswaki
 
"Hakuwa na walinzi maana waliondolewa kipindi cha sakata la Corona, sasa wakati anapanda ngazi wakashuka watu watatu wakamuambia wewe unaisumbua sana Serikali, sisi hatuna mpango wa kukuua ila tunataka tukuvunje ili ushindwe kufanya kampeni" - Msigwa Peter
Mkuu inaonekana Msigwa anawajua hao watu siyo, Wanasiasa wa Tanzania wanasiasa za kitoto Sana..
 
Uwe unatumia akili kabla hujaleta thread humu usidhani kuandika andika ovyo hakuna anayeshindwa kila mtu akiandika ovyo itakuaje?? Unataka watafute huruma kwa Magufuli? Kanywe chai toa ushenzi hapa
Punguza povu bwashe ungejikita kwenye hoja ungeeleweka zaidi, matusi hayasaidii na kwa Hali hii Ndo maana huwa mnaitwa kikundi Cha genge la wahuni maana hoja zenu mshaona Ni matusi na mapovu tu.
 
Hawa wameshaigeuza iyo ya kuvamiwa ndo sera, wananchi tumeshituka, atakaye wapa kura hakika ana maslai ya moja kwa moja nao lasihivyo hawapati kitu hapa
Nikwel mkuu

Tatizo lao kubwa Hawajui kusoma nyakati, wananchi washawachoka kwa Kiki zao za kuvamiwa kwa kisingizio Cha watu wasiojulikana
 
Unakuta aliyeandika bado hata hajapiga mswaki
Inaonekana na wewe umeamua kushare kitu kinachokuhusu mwenyewe Kupitia mgongo wa mwanaume mwenzio..

Ok ahsante kwa taarifa tumejua.
 
Tufanye kwamba amejeruhiwa katika mazingira yasiyo na walinzi wala watu wa ziada waliojeruhika ili kuthibitsha ni kweli uvamizi wa kudhuru na sio kiki.

Ndio kusema tusijadili maumivu yake??
 
Hivi ukishakuwa mwanasiasa huwezi kuwa na ugomvi na watu wengine nje ya hii sphere hadi kila unapovamiwa, kupigwa au kufanyiwa fujo ionekane ni serikali ndo wahusika?
Hapo Ndo watu tunapofeli Yani tunajikuta tunasahau kuwa Kuna maisha nje siasa na uongozi.

Na Ndo maana nikawauliza wanabodi katika Uzi wangu kuwa

"Nikweli tukio la kuvamiwa Mbowe limekaa kisiasa tu ama lipo kijamii pia"

Watu wanavyowachukulia wanasiasa utafikiri siyo wanajamii,, watu wangapi wanavamiwa? Watu wangapi wanaviziwa na kukabwa mbona serikali haihusishwi kwa hao wengine Ila wapinzani pekee?
 
Aisee umeandika upupu najuta kusoma Hii thread haina kichwa wala miguu ata sijui unatumia nini kufikiri
 
Tukio ni la kisiasa, ila inalekea kuwa wahusika siyo wanasiasa kutoka chama chochote cha siasa, na wala hawajatumwa na chama chochote cha siasa. Kuna watu wako nje ya ulingo wa siasa, ila ni mahasimu wa Serikali iliyopo madarakani, haina unafuu kwao kutokana na matendo yao!
 
Hoja dhaifu sana hizi!
Sasa unatoa hoja kama hii "
Wavamizi waliingiaingia je ndani ya eneo la nyumba ya Mbowe mpaka wakamusubiri apaki gari lake akaanza kupanda ngazi ndo wakamuvamia? Nikweli nyumba ya kiongozi mkubwa Kama Mbowe haina walinzi kweli Hadi watu waingie kirahisi vile? Na Kama wapo walipambana na hao wavamizi?"

Ni hoja gani sasa?
Kama wavamilzi waliompiga Lissu risasi waliweza kufanya hivyo tena mcha jua likiwaka na eneo lenye ulinzi wa askari 24hrs, unashangaa hili la Mbowe lililotokea usiku wa manane?
...kila kitu mnadai ni kiki za kisiasa! Yaani kiki za kisiasa mtu ajiumize na kiujivunja, hivi inaingia akilini kweli hiyo?
Yaani nyie watu mnaodai haya mambo kama haya yanayotokea ni kiki, huwa nawaona ni kama wendawazimu tu!
Mnajitoa ufahamu, huku mkivaa unafiki eti sisi ni wamoja na tunapendana!
...Matakataka kabisa nyinyi!
Siasa zitawapeleka pabaya, miaka 10 ijayo unaweza kuwa tayari ushatafunwa na funza, hujui kesho yako, jivike ubinadamu!
 
Ifike mahali chadema ichunguzwe kwa jicho la pili maana matukio yao yote yana dalili za inner circle.

Ni wazi inatafutwa kick nyingine hapa ila nadhani watanzania tumeamka sasa!
 
Watanzania shida sana,sasa kuandika uharo huo ndiyo nini,mimi zamani sana wakati niko mdogo kuna mambo mengi sana nilikuwa najiulizaga harafu sielewi, majibu,tuondolee siasa
 
Back
Top Bottom