Viongozi wa CHADEMA msitafute huruma ya wananchi kupitia kiki za matukio, mtaumia bure

Hakuna mtu ataamini kitu kama hiki yani watu watumwe kuja kufanya tukio kama hilo halafu wao wenyewe wajitaje namna hiyo??

Halafu kama alikuwa peke yake hiyo kauli huyu Msigwa aliitoa wapi?? Yeye kasimuliwa na nani hizo kauli??

Mchungaji mzima unakuwa mnafiki kiasi hiki kwanini lakini??
 
Hivi wewe unaweza kujishambulia ili upate sympathy ya watu ?
 
Ifike mahali chadema ichunguzwe kwa jicho la pili maana matukio yao yote yana dalili za inner circle.

Ni wazi inatafutwa kick nyingine hapa ila nadhani watanzania tumeamka sasa!
Wewe inamaana hao watu polisi imeshindwa kuwagundua,kwa matukio yote hayo Wewe mwenye akili ndo ugundue,sisi wapenda amani na si wapenda siasa,tunapenda wanaofnya hivyo polisi iwakamate,au we ka unawajua nenda kawaambie polisi,au Wewe unakili kuwa wanaofanyaga hayo matukio wanauwezo wa hali ya juu kuliko polisi?msipende kuingiza siasa kwenye kila kitu ,mtaiharibu tanzania,
Tanzania kwanza,mivyama yenu baadae
 

Mbona mimi nimeamini!
Mimi siyo mtu? Sasa kama unabisha na kukataa leta ukweli sasa!
Wanafiki ni nyie ambao inaonekana mmefurahia! Roho nyeusi kama panya....
Wazandiki wakubwa!
 
Hapo hujajibu hoja yoyote ya mtoa mada mkuu.

Hivi we kwa akili za kawaida tu unadhani serikali ni wapumbavu kiasi hicho hadi wafanye tukio kama hilo tena kipindi kama hiki cha fukuto la uchaguzi wakati wanajua kabisa litashtua watu wengi na watatia shaka??

Hawawezi kuwa wajinga kiasi hicho hata kidogo, tena jana Lissu katoka kuongea alafu leo wamshambulie mtu namna hiyo??

aah hapana na kama ni hivi basi watakuwa hawana akili kabisa hata moja kichwani.

Alafu mbaya zaidi heti wanajitaja kabisaa eti wewe ndio unamsumbua Rais tumekuja kukuvunja!!!!
Hakuna atakae amini ujinga kama huu.
 
Ifike mahali chadema ichunguzwe kwa jicho la pili maana matukio yao yote yana dalili za inner circle.

Ni wazi inatafutwa kick nyingine hapa ila nadhani watanzania tumeamka sasa!

Vyombo vya ulinzi na usalama vipo!
Kama kiki basi wakamate hao wanaodhaniwa kufanya hivyo, wanashindwaje kuwakamata???? Moroto alisema Dom pako safe, sasa haya yanatoka wapi? Kama ni watu wanataka kuichafua Dom na serikali basi watafutwe wakamatwe sheria ichukue hatamu, na siyo kuja na poroja za kiki hapa!
Ooh mara mhusika ameshindwa/amekataa kutoa ushirikiano... basi hatuwezi kuendelea na upelelezi!
Blali shit...[emoji35][emoji35]
 
Mkuu wahusika wenyewe ndiyo hao hao. Wakishatenda ushetani wao hukimbilia kutoa lawama za kipuuzi. Lakini DAWA yao yaja tusijekulaumiana huko mbeleni.
 
Mbona mimi nimeamini!
Mimi siyo mtu? Sasa kama unabisha na kukataa leta ukweli sasa!
Wanafiki ni nyie ambao inaonekana mmefurahia! Roho nyeusi kama panya....
Wazandiki wakubwa!
Mkuu rudia tena hiyo post yangu kisha toa ufafanuzi kwa maswali nilio uliza hapo alafu ndo tuendelee kujadili kama huna majibu ya maswali yangu basi hatuna haya ya kujibizana tena.
 

Sijacomment kujibu hoja, na wala sihitaji kujibu hizo hoja maana na za kipuuzi zote, hamna hoja ya msingi hata moja!!
Whatever iwe serikali, iwe wahuni au ni yeyote basi ufanyike mchakato upesi hao wahusika watiwe mbaroni!
Mambo ya kubwabwaja ooh, sijui siyo serikali, mara ni wahuni au ni cdm wenyewe kwa wenyewe ndio wamefanya ili kutafuta kiki ni mambo yanayochosha kusikia!
Haiwezekana ishu kama hizi kutokea halafu zipite kama upepo, hata anayehisiwa asikamatwe!
...hili kwa mfano likipita, basi tujiandae kwamba lingine kubwa zaidi laweza kutokea!
Haya mambo yanaleta hofu kwa raia na viongozi, hasa wa vyama pinzani!
Why, haya yatokee kipindi hiki....
 
Mkuu utahangaika sn na CHADEMA ila ujue kitu kimoja...
CHADEMA IPO KWENYE MIOYO YA WATZ wkt ccm ipo kwenye mioyo ya polisi na tume ya uchaguzi
 
Uwe unatumia akili kabla hujaleta thread humu usidhani kuandika andika ovyo hakuna anayeshindwa kila mtu akiandika ovyo itakuaje?? Unataka watafute huruma kwa Magufuli? Kanywe chai toa ushenzi hapa
Ndio ushamalizana naye hapo hata kama kaandika utumbo basi mpe ndizi ili ale ndizi utumbo sasa wewe unaamua kuutupa kabisa utumbo wake kitu kinachopelekea uonekane wewe una roho mbaya
 
Mkuu wahusika wenyewe ndiyo hao hao. Wakishatenda ushetani wao hukimbilia kutoa lawama za kipuuzi. Lakini DAWA yao yaja tusijekulaumiana huko mbeleni.

Si wakamatwe wafikishwe mbele ya sheria?
Kama unawajua kwa nini usiwataje hadharani au hata huku jf wakajulikana then sheria ikachukua hatamu??
Mambo ya kusema ni hao hao, wanafanya na kutoa lawama hizo ni story za mtaani tu!
...unawajua wahusika wataje, au niambie kama unavielelezo vya ushahidi niwaanike hadharani pasipo kujali chama wala nini!!
 
Mkuu rudia tena hiyo post yangu kisha toa ufafanuzi kwa maswali nilio uliza hapo alafu ndo tuendelee kujadili kama huna majibu ya maswali yangu basi hatuna haya ya kujibizana tena.

Kumbe tunajibizana boss..!!
Haya, ngoja nikae kushoto!
 
Spika wa Bunge Job Ndugai alitamka hadharani kuwa Mh Mbowe hatorudi Bungeni mwezi oct. mwaka huu baada ya Uchaguzi Mkuu. Alikuwa na maana gani?? Anza nae huyo.
 
Hoja za kipuuzi ni kwa kipimo kipi ulichutumia kuzipima??
Na hizi zako umezipima kwa kipimo gani hadi ukaona sio za kipuuzi??

Ukakasi tunao ujadili ni wa jinsi tukio lilovyo tokea na tuhuma zinazotupwa kwa serikali kuwa ndio wahusika.

Wakikosekana kukamatwa pia sio Jambo la kushangaa kwasababu matukio kama hayo hayawakuti wanasiasa tu bali watu wengi wamekubwa na matukio kama hayo na wahusika bado hawajapatikana sa sio ajabu kwa mh Mbowe tu.

Unasema kwanini yawe kipindi hiki tu
Kwani kina Chacha Wangwe walikufa kipindi gani?
Kina Mwangosi yaliwakuta kwenye kipindi gani?
Dr Ulimboka aling'olewa kucha kwenye kipindi gani?
 
Punguza povu bwashe ungejikita kwenye hoja ungeeleweka zaidi, matusi hayasaidii na kwa Hali hii Ndo maana huwa mnaitwa kikundi Cha genge la wahuni maana hoja zenu mshaona Ni matusi na mapovu tu.

Hoja yako wewe iko wapi hapo? Au nilichokiandika we hujakilewa? Ndio nyie mnafanya watanzania wote tuonekane wajinga
 
Nikwel mkuu

Tatizo lao kubwa Hawajui kusoma nyakati, wananchi washawachoka kwa Kiki zao za kuvamiwa kwa kisingizio Cha watu wasiojulikana
Achenj viburi vyenu aisee..tatizo la waafrika tunaangalia leo tu....hivi hujui wewe unaweza ukapata watoto ambao wakawa chadema au wajukuu zako...au wana ukoo wako....?
Yanapotokea mambo maovu yakemewe kwa nguvu zote....haijalishi kapata matatizo mtu wa CCM, CHADEMA, TLP,ACT etc.....

Hii tabia yenu ya kuchukulia poa na kufanya siasa kwenye matatizo yanayotokea upinzani ndo yanaharibu siasa za nchi yetu
 
Kumbe tunajibizana boss..!!
Haya, ngoja nikae kushoto!
Wewe ndio unaye puyanga ovyo bila kujibu maswali ninayo uliza, angalia kwenye quote zako kuna hoja yoyote nilio itoa ulio ijibu mkuu?? Jifunze kujibu hoja na sio kuandika chochote tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…