Kwamba tangazo limetoka kuwa mrudishe vyeti vya usajili vya kudumu mpewe vya miaka mitano mitano! Hamjashtuka bado? Mpo usingizini bado?
Mkiamka mtakuta mmefutwa. Serikali inaona njia rahisi ya kufuta usajili wa Kanisa kama la Gwajima na makanisa yale wasiyotataka ni hiyo.
Waliwahi kutishia Kanisa Katoliki wakati walipotoa waraka wa Kichungaji, wakatishia KKKT nao walipotoa waraka wao wa Pasaka.
Maana yake kama wangelikuwa wameshafutia makanisa yote usajili wa kudumu kama wanavyotaka kufanya na kutoa vibali vya miaka mitano, makanisa hayo yangelishafutwa.
Kuna wakati walikuwa na mgogoro mkubwa na Kanisa la Askofu Kakobe. Kwa mtindo wa vibali vya miaka 5 lingeshafutwa kirahisi. Unanyimwa tu kibali kipya.
Nilikuwa nafikiri ningesikia makelele kutoka kwa maaskofu lakini kimya.
Sio taasisi za dini ya Kikrsto tu, hata Waislamu pia. Taasisi kama za Shehe Ponda itakuwa rahisi kuzifuta kwa kuwanyima kibali cha miaka 5 mingine.
Huu ni mpango muovu sana kwa taasisi za dini. Ni mpango wa kidikteta wa hali ya juu sana ambao sijausikia hapa Afrika. Watumishi wa Mungu mnatishwa muogope kuikosoa serikali kwa kuogopa kuwa mtanyimwa vibali vya miaka 5.
Ukishafutwa kusajiliwa tena itakuwa ngumu.
Nilikuwa nategemea kusikua TEC, CCT, CPCT, BAKWATA, n.k. wakilisemea hili kwa nguvu zote.
Usajili ubaki kuwa wa kudumu, sio kuufuta na kutoa vibali vya miaka 5. Nilimweleza Padre wangu hilo akasema atalipeleka ngazi za juu lakini sijasikia likisemwa.
SHITUKENI!