Nuraty J
JF-Expert Member
- Sep 18, 2018
- 1,724
- 3,834
Dar es Salaam. Viongozi wa dini nchini wamewaasa Watanzania watakaomkosoa Rais Samia Suluhu Hassan wawe tayari kutoa ushauri wa nini kifanyike ili aendelee kuliongoza vyema Taifa na kufikia maendeleo katika utawala wake.
Wito huo umetolewa Jumamosi, Juni 26, 2021 na viongozi wa dini katika kongamano la kumuombea na kumshukuru Mungu kwa siku 100 tangu kiongozi mkuu huyo wa nchi alipoapishwa Machi 19, mwaka huu.
Waliyasema hayo jana, baada ya kumalizika kwa kongamano hilo ambapo, Shekh Haruna Jumanne; Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe na Mchungaji Yaspi Bendera kutoka kanisa la ufunuo, waliokuwa miongoni mwa viongozi waliongoza maombi hayo.
Walisema katika siku zake 100, Rais Samia kupitia hotuba zake mbalimbali ameonyesha njia nzuri kwa kufungua milango kwa Watanzania kumshauri na imemsaidia, kwani imejenga imani kwa Watanzania wengi hata wale waliodhani asingemudu jahazi hilo.
“Mwanzo wake umekuwa mzuri ameonesha sifa ya kiongozi, ni wakati wa kila Mtanzania kujifunza kwanza kwa kumuombea afya njema, lakini kukosoa na kuonesha njia ni muhimu kwa kuwa ndio msingi wa kujenga Taifa bora lenye furaha,” alisema Askofu Kakobe.
Alisema kuongoza nchi sio kazi rahisi na Rais Samia anakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya kujenga Taifa hasa wakati huu ambapo kuna tishio la wimbi la tatu janga la virusi vya corona.
“Sio jambo dogo kila mmoja wetu anatakiwa kumuombea kwani, ili ashinde anahitaji ushauri bora wa kuyakabili kwa kuwa tatizo ni la kidunia sio nchi,” alisema.
Askofu Kakobe alisema anaamini changamoto anazopitia ikiwemo corona itapita na kumuomba Rais Samia kuzidi kumtanguliza Mungu kwenye majukumu yake.
Naye Sheikh Jumanne: “Viongozi wa dini tumekusanyika katika kongamano hili bila kujali itikadi zetu, kumuombea Rais Samia ili Mungu amsaidie afya njema aweze kutimiza majukumu yake na wananchi wote tunatakiwa kumuunga mkono,” alisema Shekh Jumanne.
Mchungaji Yaspi alisema Rais Samia ameanza kazi nzuri katika utawala wake hivyo, ni wakati wa Watanzania kuombea azidi kuota maono mema kwa maslahi ya Taifa.
“Ni wakati wa kufunga maombi kumuombea azidi kuota maono mazuri ya kulijenga Taifa letu kwa kufikia maendeleo ambayo kimsingi wote tunataka kuyaona,” alisema Mchungaji Yaspi.
Aliongeza kuwa viongozi wanaomsaidia na wale wa kisiasa na kidini ni wakati wa kumuunga mkono kwa kutoa mawazo mbadala yenye kulijenga taifa kwa niaba ya wananchi wote. “Viongozi tunachukuliwa kama vioo kwenye mambo mbalimbali na tunayo nafasi ya kutoa mchango wa mawazo utakaomsaidia Rais na wasaidizi wake kutimiza majukumu waliyonayo,” alisema.
Katika Kongamano hilo walijitokeza viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe pamoja na wananchi wengi kuliombea taifa na Rais Samia.
Chanzo: Mwananchi