Viongozi wa Dini nyingine mpo wapi kukemea maovu yanayoendelea?

Viongozi wa Dini nyingine mpo wapi kukemea maovu yanayoendelea?

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
Kumekuwa na Mambo mengi ya ovyo hapa Nchini.

Viongozi wengi wa Dini wamejitokeza hadharani kukemea maovu hayo, lakini kuna viongozi wa Dini nyingine wapo kimya kana kwamba hawayaoni yanayoendelea.

Naomba hawa viongozi wa Dini nyingine waliokaa kimya watuambie, wapo upande gani?

Je, wanahusika katika mikasa hii?

Waandishi wa habari, ebu nendeni kwa viongozi hawa wa Dini nyingine ambao wameamua kukaa kimya wakati Watanzania wanapitia katika mateso na waulizeni kuwa, Je, wao hawaoni yanayoendelea?
 
Wanajitokeza mahara penye maslahi yao, kama issue ya bandari walijitokeza wako kifedha zaidi sio maadili.
 
"Dini nyingine" waumini wake ni akina nani? Wewe kama umeshindwa kuzitaja hizo dini una mamalaka gani ya kuwalaumu wengine. Huna tofauti na hao unaowalaumu
 
"Dini nyingine" waumini wake ni akina nani? Wewe kama umeshindwa kuzitaja hizo dini una mamalaka gani ya kuwalaumu wengine. Huna tofauti na hao unaowalaumu
Hapo inaonekana wewe ndo upo kwenye hizo Dini nyingine.
 
Taasisi za dini zinazojielewa zina kemea au kupongeza jambo baada ya kutumia vyombo vyao vya kitafiti kujiridhisha na hicho wanachopaswa kukikemea au kukipongeza...

hawazingatii ramli, ushirikiana, huruma au hisia za wanaharakti wasaka tonge ambazo nyingi ni uzushi na uongo tu 🐒
 
Back
Top Bottom