Watanzania wametakiwa kulinda, kutunza amani na utulivu hasa kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani utakaofanyika mwakani.
Viongozi wa dini ya Kiislamu wametoa rai hiyo kwenye kongamano na dua maalumu ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan iliyoandaliwa na mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, kwa ushirikiano na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) wilayani humo.
Dua hiyo iliyofanyika jana Desemba 14, 2024 katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkuranga ilitanguliwa na Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika asubuhi yaliyowakutanisha masheikh wakiwemo wa mikoa ya Arusha, Kigoma, Kagera, Dar es Salaam na Pwani.
Maulid hayo yalibeba kaulimbiu ya 'Tulinde maadili yetu na amani yetu kwa masilahi ya Taifa letu'.
Watanzania wamesisitiziwa kuitunza na kuimarisha amani iliyopo ili kuunga mkono jitihada za Rais Samia aliye mstari wa mbele kuihubiri, akikemea mmomonyoko wa maadili akiwataka viongozi wa dini kuungana na Serikali kusimamia suala hilo.
Watanzania kama watanzania hakuna anaevuruga amani hata pale wanapozurumiwa haki zao kwa kupachikiwa viongozi ambao hawakuwa chagua kwa kupitia kura fake wanakuwa wapole kwa ajili ya kulinda amani ya nchi.
Mchawi wa amani ya Tanzania na ambaye hawataki kumsema ni CCM na serekali yake kwa dhulumu haki za wananchi.