Watu wanadhani katiba ndio inaongoza nchi wakati katiba hiyo hiyo inatengenezwa na kusimamiwa na watu hasa wanasiasa, kama taifa inatakiwa tutengeneze wanasiasa wazalendo na raia wazalendo na wenye weledi mkubwa, lakini tukiendelea kuwa na wanasiasa ambao leo wanasema hivi mara kesho vile, leo wanaamini hichi kesho wanageuka, leo wanasema fulani fisadi kesho wanasema msafi, hata tuwe na katiba nzuri kiasi gani hatutasonga mbele.