Viongozi wa Dini wakemee pia Uharibifu wa Mazingira wanapohimiza watu waache dhambi ili mvua zinyeshe

Viongozi wa Dini wakemee pia Uharibifu wa Mazingira wanapohimiza watu waache dhambi ili mvua zinyeshe

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Pichani ni mti niliokuta umekatwa sehemu ambayo hakuna miti kabisa na kuna shule ya sekondari. Na pia eneo ambalo mti ulikuwepo sio hata uwanja wa mpira. Mimi kama mpenda mazingira nikajiuliza maswali mengi sana yanayoweza kuwa sababu ya kukata huu mti nikakosa sababu yenye mashiko. Nimepanga nikutane na wahusika wanipe sababu zao. Ukataji wa miti kama huu ni aina mojawapo ya uharibifu wa mzingira hali inayoleta athari kubwa kwenye upatikanaji wa mvua.

Tangu utotoni nimekuwa nikishuhudia jamii ikifanya maombi kwa imani mbalimbali ili mvua zinyeshe. Wakristo, waislamu na waabudu mizimu kwa pamoja kila imani kwa wakati wake tumekua tukifanya maombi kwa Mungu kuhusu mvua. Hili ni jambo jema sana kwasababu kupitia hayo maombi ni kweli mvua hunyesha. Mwaka 1994 nilishuhudia muujiza mkubwa sana ya mvua kubwa kuanza kunyesha ghafla wakati maombi yakiendelea makanisani.

Lakini kupitia uzi huu niwaombe viongozi wa dini wasiishie tu kusema tuache dhambi ili mvua zinyeshe. Ninawaomba wakemee pia uharibifu wa mazingira unaofanywa na watu. Kuna watu sio wazinzi, walevi au wezi lakini utakuta wanakata miti hovyo au kwenda kunywesha mifugo kwenye chanzo cha maji. Mtu anaweza asiwe msengenyaji lakini utakuta anafanya shughuli za kilimo kwenye chanzo cha maji.

Pamoja na kukemea dhambi nadhani hawa viongozi jinsi walivyo na ushawishi wakashiriki kukemea vitendo viovu vya uharibifu wa mazingira itasaidia sana. Kwa mfano viongozi wa dini wakisema kila muumini apande angalau mti mmoja kwenye nyumba yake hakika miti mingi mno itapandwa. Viongozi wa dini wakikemea waumini kutofanya shughuli kwenye vyanzo vya maji nadhani itasaidia.

20220911_153405.jpg
 
Welldone mpenda mazingira kudos kwako, sasa tujadili hili miti zaidi ya 2500 inakatwa kule Selous Game Reserve ili HEP station ijengwe, je umeshawahi kuiona au kusikia environmental report ya mradi ule, kuna mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania, ripoti ya mazingira umeiona au kuisikia? (report zote hizi zipo kwenye public domain, ni haki yetu ziwe wazi).

Je, kweli jiji la Dar hadi miaka hii halina mpango dhabiti kuhusu issue ya maji wakati jiji linakua siku hadi siku, why tufanye kazi kama fire brigade? Tanzania ina 3 major fresh water lakes, tunayatumia yale maji kivipi?suala la maombi ni la kiimani, binafsi mizimu ndio yangu.
 
Welldone mpenda mazingira kudos kwako, sasa tujadili hili miti zaidi ya 2500 inakatwa kule Selous Game Reserve ili HEP station ijengwe, je umeshawahi kuiona au kusikia environmental report ya mradi ule, kuna mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania, ripoti ya mazingira umeiona au kuisikia?(report zote hizi zipo kwenye public domain, ni haki yetu ziwe wazi),je kweli jiji la Dar hadi miaka hii halina mpango dhabiti kuhusu issue ya maji wakati jiji linakua siku hadi siku,why tufanye kazi kama fire brigade?,Tanzania ina 3 major fresh water lakes, tunayatumia yale maji kivipi?suala la maombi ni la kiimani, binafsi mizimu ndio yangu
Kiukweli kuhusu Selous nalaani mno ule mradi kwasababu option ya umeme wa gesi ilikuwepo. Ule uharibifu utakuwa pia umesababisha vifo vya wanyama wengi. Je, kama nchi kuna hatua gani tunachukua kwa athari zilizotokea? Watu wa mazingira tulio nao ni wa mchongo sana. Kwenye kampeni zao utaona ni kwenda kufanya usafi coco beach na kuvaa tshirt zenye kauli mbiu.
 
Back
Top Bottom