Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini wamekutana wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro kufanya ibada maalumu eneo kulikotokea ajali iliyoua watu 42 na wameiomba Serikali kuweka mnara wa kumbukumbu wenye majina ya waliofariki katika eneo hilo kama moja ya njia ya kuhifadhi historia
Wamesema mnara huo utakuwa pia sehemu ya maombi na kutafakari kwa familia, jamaa na wananchi kwa ujumla, sambamba na kuelimisha kuhusu umuhimu wa usalama barabarani.
Ajali hiyo ilitokea Juni 28, 2025 katika eneo la Sabasaba, Same mjini ikihusisha basi Kampuni ya Chanel One lililokuwa likitokea Moshi kwenda Tanga na basi dogo aina ya Coaster lililokuwa likitokea Same Mjini kwenda Moshi kugongana uso kwa uso na kuwaka moto wakati abiria wakiwa ndani ya magari hayo
Waliofariki katika ajali hiyo jumla yao ni watu 42, ambapo kwenye gari dogo aina Coaster walifariki watu 31 waliokuwa wanakwenda harusini mjini Moshi, huku kwenye basi la Chanel one wakifariki watu 11
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa Juni 29, alisema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa tayari ya basi la Kampuni ya Chanel One na kupoteza mwelekeo na kwenda kugongana uso kwa uso na Coaster iliyokuwa imebeba watu hao ambao walikuwa wanakwenda kwenye sherehe
Akizungumza mara baada ya kufanyika ibada hiyo ya maombi, Kaimu Sheikh Mkuu wa Wilaya hiyo, Abbas Hassan amesema kama viongozi wa dini wataendelea kufanya maombi maalumu katika eneo hilo na wilaya hiyo nzima ya Same ambayo imekuwa ikikumbwa na matukio ya ajali
Mchungaji wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Amani Mndeme amesema wataendelea kufanya maombi kila mara kuzunguka maeneo ya wilaya hiyo kwa kuwa kumekuwepo na matukio mengi ya ajali
Katibu wa umoja wa dini mbalimbali wilayani humo, Elizabeth Mchani amesema kila baada ya mwezi wilaya hiyo inakuwa na matukio ya ajali, hivyo akasema ni wakati sasa wakumuomba Mungu atakase wilaya hiyo