the ultimatum
JF-Expert Member
- Dec 16, 2012
- 403
- 116
Walichokifanya hawa masheikh wa mandera Tanzania hufanywa most of the time na Mkuchika kila wanapoona habari fulani inatishia masilahi ya uwepo wao. Kama lengo ni kuzuia DSTV kwa sababu inaonesha picha za ngono basi wana sababu za kufanya hivyo na ilitakiwa DSTV wawe wana filter vipindi ambavyo haviendani na maadili ya sehemu wanazofanyia biashara. Kama ku-block porn related progrmmes. Ila kama hawa jamaa wamefanya hivyo kwa sababu za kutaka jamii isiangalie programme kama mipira etc. watakuwa wamefanya makosa makubwa sana. Ila kinachotakiwa hapa ni serikali kukaa na hawa Masheikh kukubaliana jinsi ya kundesha vipindi bila kuaribu maadili ya watoto na hasa kuonesha ngono kwenye TV. Kazi ya watumishi wa mungu ni kushauri ila siyo ku-enforce hiyo ni kazi ya serikali na sheria zilizopo
Inawezekana ukawa sahihi, lakini tujiulize katazo hilo ni sahihi kwa ulimwengu wa sasa?
Kwanini walitoe katazo hilo kwa Dstv, huku ikijulikana fika matumizi ya Dstv hayajafika kwa familia nyingu za afrika mashariki! Ni familia chache sana ambazo zinatumia Dstv.
Je, wamefanya jitihada nyingine za ziada kama kukataza usambazaji wa CD za ngono? Au wanaishia kutoa makatazo ya Dstv pekee?
Na je, vipi kuhusu kumbi za starehe na maeneo mengine ambayo yamekuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili?
Vipi kuhusu vipindi vya televisheni vya ndani ambavyo vimekuwa vinaonyesha mambo yanayoharibu maadili. Sio lazima ngono tu lakini hata kuikaribia ngono katika uislamu ni kukiuka maadili ya uislamu.
Ninachotaka nieleweke hapa ni kwamba, ulimwengu sasa umebadilika sana. Kunavyanzo vingi sana vya kupatia taarifa. Leo hii utakataza matumizi ya Dstv lakini je utakataza na matumizi ya internet?
Leo hii kuna sites nyingi sana zinazoonyesha picha za ngono. Kama mtoto ana hobby ya kuangalia porno bila hata ya Dstv ataweza kuziangalia tu.
Sisemi tusizuie matumizi ya Dstv, ila napenda tuangalie lengo la kukatazwa kwake. Ni jambo jema kukataza matumizi ya Dstv kwa kigezo cha maadili, nami naunga mkono. Lakini tujiulize maadili yanavunjwa na Dstv peke yake?
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kutoa elimu kwa umma, hasa watoto na vijana kuhusu mmomonyoko wa maadili na hasara zake, hii ndiyo suluhisho pekee.
Hata hivyo uonyeshwaji wa porno kiholela kama maeneo ya entertainment centres unapaswa upigwe marufuku knowing that inachochea kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili. Lakini pia serikali iweke sheria juu ya usambazaji holele wa CD za ngono.
Lakini pia elimu kwa umma ni jambo muhimu zaidi.