DOKEZO Viongozi wa Halmashauri ya Mji Masasi ni tatizo, Mkurugenzi huyu anawaonea watu

DOKEZO Viongozi wa Halmashauri ya Mji Masasi ni tatizo, Mkurugenzi huyu anawaonea watu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Mimi nina jambo natamani kuchangia lijulikane kwa umma, imekuwa ni kawaida sana kwa Watumishi wa Serikali hasa katika Halmashauri ya Mji Masasi kuwahudumia Wananchi hovyo na kwa uonevu.

Inapotokea mwananchi akaenda kwa Mkurugenzi wengine wanatushiwa hadi kuwekwa ndani ilimradi tu Mkuu awalinde watu wake.

Kikubwa zaidi juzijuzi hapa kuna kesi Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji aliwaweka ndani vijana wawili wa miaka 21 alikuwa akigombania nao mwanamke!

Vielelezo vyote vipo nakala ya hukumu, hati barua ya wazazi wa watoto hao walioandika kwa Hakimu wa Mkoa kulalamika juu ya hili.

Hizo hapo ni hati ya hukumu, yaani walikamatwa tarehe 18 Jumamosi kisha Jumatatu wakafungwa bila kuwepo mashahidi wala upelelezi!

Namna ambavyo kiongozi huyo anatumia vibaya madaraka, kisha dada aliyetajwa humo siye mhusika, mhusika ni mtumishi katika Halmashauri yake jina nitawatajia.

Malalamiko.jpg


photo_2023-02-15_13-38-08.jpg


2.jpg


3.jpg


4.jpg

5.jpg

Gereza.jpg
 
Daaah una jua mimi ni nani?

Ila huyu mkurugenzi sijui, tusiongee mengi ila mama atusaidie kwa huyu jamaa aisee

Enzi ya mwalimu alikataa maneno kama haya ya kuiweka serikali mfukoni, mfuko wako una ukubwa kiasi gani? Wewe ni nani mpaka uweke watu mfukoni?
 
Kaka Pascal Mayalla kwa heshima yako, tusaidieni hizi jamii zinazo kandamizwa na wachache kwa madaraka yao waliyo pewa

Huku wakijinasibu kwa mujibu wa wadau kuwa hakuna wa kuwa fanya kitu
 
Aisee kama hukuwahi kuoneshwa dharau basi tembelea Halmashauri ya Masasi..

Kuna Afisa mmoja alifukuzwa mwaka juzi sasa mwaka jana nilitembelea ofisini hapo namkuta kaimu kaweka miguu juu ya meza anasikiliza nyimbo za harmonize, kabla hajanifahamu alikuwa anajibu kwa kejeri kuliko ata secretary niliyemkuta mlangoni.....
 
Hawa ndio wakurugenzi waliotumwa na rais kuja kishughulikia wananchi,na hayo anayaoyafanya ndio maelekezo kutoka kwa bosi wake (rais).
 
Huyu mkurugenzi ni mtu wa hovyo sana sijui kwanini mpaka leo bado yupo masasi.
Kwanza tangu awekwe pale hata maendeleo hakuna kabisaa
Sijui ni nani yupo nyuma yake
 
Back
Top Bottom