KERO Viongozi wa Idara Morogoro hawajauelewa vizuri Mfumo wa PEPMIS, tunaumia sisi Watumishi wa chini

KERO Viongozi wa Idara Morogoro hawajauelewa vizuri Mfumo wa PEPMIS, tunaumia sisi Watumishi wa chini

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Serikali ilinzisha Mfumo wa Public Employee Performance Management Information System – PEPMIS lengo likiwa ni kurahisisha utendaji kazi na kuweka uwazi kwa kuwa inajulikana wazi suala la Urasimu ndani ya Taasisi za Serikali zipo kwa kiwango cha juu.

Kwa wenzangu ambao hawafahamu, Mfumo huu wa PEPMIS umeunganishwa na mifumo mingine kama vile Mfumo mpya wa Taarifa za Usimamizi wa Rasilimali za Watu (HCMIS) na mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) hivyo kurahisisha upatikanaji wa taarifa za wafanyakazi, kurahisisha michakato mbalimbali.

Pamoja na maufaa hayo ya mfumo huo, sisi baadhi ya Watumishi wa Serikali Mkoani Morogoro tuna changamoto ya kutotendewa haki katika matumizi ya Mfumo PEPMIS.

Kwanza kabisa mfumo unawasumbua watu jinsi ya kuutumia, bado kuna Watumishi wengi hawajui jinsi ya kuingiza taarifa kwa usahihi.

Kuna wengine walitakiwa kusimamiwa na Supervisor lakini wasimamizi hao hawatimizi jukumu lao, matokeo yake mfumo ulipomalizika mwaka husika wa Kiserikali, utendaji wa Watumishi ukawa unasoma 0 au chini ya 50%.

Tatizo moja kubwa lilianzia kwa wale walioenda kufundishwa junsi ya kuutumia mfumo, wengi wao hawakuuelewa vizuri, hivyo kama wao wameshindwa kuuelewa inaaanisha wale wa chini yao itakuwa ngumu pia kuuleewa au wao wasimamizi (Supervisors) wanashindwa kutimiza majukumu yao inavyotakiwa.

Unajua kiongozi wako kukwambia live kuwa alienda kwenye mafunzo kisha hakuelewe, ni jambo gumu.

Mfano HR ndiye anatakiwa kusimamia wtendaji wote wanaojaza kwenye mfumo huo, lakini wapo ambao (HR) hawajui au wanafanya makusudi.

Matokeo ya hayo yote yamesababisha mwaka wa Kiserikali umepita, hatujaongezewa mshahara, hakuna mabadiliko yoyote pia, alama za watumishi zinaonekana chini kuliko uhalisia.

Hata tulipojaribu kukata rufaa tayari mfumo ulikuwa umeshafungwa tangu Agosti 7, 2024.

Pia soma ~ Hasara za PEPMIS kwenye haki za watumishi
 
Back
Top Bottom