Mngetulia kwanza mkajipanga, huku kukurupuka ili mradi kushindana na jamii ya mitandaoni ndo kutazidi kuwatoa relini.
Jana mzee wa Miga katoa tamko bila kuwasiliana na CHADEMA kujua kinachojiri.
Leo wanamama wameapishwa huku kiongozi wao akimtaja Mwenyekiti Mbowe. Kesho Makene au Mnyika atakurupuka kuongea, keshokutwa atakuja Mbowe kuwapongeza wanamama walioapishwa leo.
Wanachama mtabaki kila mtu ananena kwa lugha yake. Yote kwa yote mnaowaamini wanasiasa endeleeni, Ila hatutachoka kuwaambia sio Lissu, Mbowe, Mnyika wala nani wote wachumia matumbo tu.