Taarifa ya kusikitisha kidogo kutoka Kata ya Mwana-Mutombo Kijiji cha Mwasinasi Tarafa ya Nkololo Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, Diwani kwa jina la Rambo Kidiga anatuhumiwa kuozesha wanafunzi wawili wa kidato cha pili na pia yeye binafsi kufunga ndoa na mabinti wawili wakisadikika kuwa ni Wanafunzi mmoja wa kidato cha pili na mwingine wa kidato cha tatu (majina yamehifadhiwa).
Halikadhalika mtendaji wake wa kijiji alifahamika Kwa jina la Bw. Magobeko mwenye umri wa miaka 50 ameozesha binti wa kidato cha pili na vilevile Mwenyekiti wa kijiji afahamikaye kwa jina la Madereke Ngoro anatuhumiwa kuoa binti wa darasa la nne na kuachishwa masomo yake
Katika Hali ya kusikitisha tumepokea malalamiko Kwa mama mzazi (Mama Nkwabi) wa binti mwanafunzi aliye sadikika kuolewa na Diwani. Rambo Kidiga huyu anaiomba serikali imsaidie binti yake aweze kurudi shuleni kuendelea na masomo yake na wahusika wafuatiliwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya ukatili hii Kwa watoto wadogo.
Ukweli wa taarifa hii upoje?

- Tunachokijua
- Baada ya JamiiForums kuchunguza Suala la viongozi katika Kata ya Mwaumatondo Kijiji cha Mwasinasi, Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu kutuhumiwa kuoa na kuozesha watoto wa shule tumepata taarifa zifuatazo:
Tuhuma za Diwani
Vyanzo kutoka Kijiji cha Mwasinasi pamoja na taarifa za Mtendaji wa Kijiji cha Mwasinasi, Shigela Masanja ni kuwa Diwani wa Kata ya Mwaumatondo, Rambo Kidiga ni kweli alimuoa msichana huyo lakini ni tukio la miaka mitatu iliyopita.
Msichana aliyeolewa alikuwa Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwaumatondo, inadaiwa alifeli mtihani wa kidato cha pili, alipotakiwa kurudia darasa akagoma na kuamua kuacha shule ndipo akaolewa na Diwani Kidiga na kwa sasa msichana huyo ni mama wa Watoto wawili.
Sauala hilo lilifika kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa wakati huo, Festo Kiswaga ambapo baada ya uchunguzi ikabainika msichana aliacha shule ndio maana hatua hazikuchukuliwa.
Diwani aelezea
Alipoulizwa Diwani Rambo Kidiga amesema “Alikataa shule wazazi wake wakaniomba nimuoe, wakanitaka niwape ng’ombe, nikafanya hivyo kwa kuwa nina utajiri wa ng’ombe. Huyo binti ni mke wangu wa 9, nimezaa naye Watoto wawili lakini jumla nina Watoto 48.
Tuhuma za Mwenyekiti
Mwenyekiti wa Kijiji, Madereke Ngoro anayedaiwa kuoa mwanafunzi wa darasa la nne, uchunguzi umebaini ni kweli alimuoa binti huyo Mwaka 2021.
Inadaiwa msichana huyo naye aliacha shule baada ya kuwa mtoro kwa muda mrefu.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwasinasi, Mikael Makaranga, anasema Msichana huyo baada ya kufeli mtihani wa Darasa la Nne hakuendelea na masomo, kauli ambayo imeungwa mkono na Mtendaji wa Kijiji cha Mwasinasi, Shigela Masanja.
Tuhuma za Mtendaji
Mtendaji wa Kijiji Mwasinasi, Shigela Masanja anayetuhumiwa kumuozesha Mtoto wake ambaye ni Mwanafunzi wa kidato cha pili uchunguzi umeonesha taarifa hiyo ni ya ukweli.
Hata hivyo Mtendaji wa Kata ya Mwaumatondo, Shedrack Lanya, yeye anasema kuwa mambo yote ambayo viongozi hao wametuhumiwa yana ukweli na yeye ameyafanyia kazi kwa kufisha taarifa kwa viongozi wa juu.
Mtendaji wa Kata ya Mwaumatondo anadai matukio ya unyanyasaji wa kijinsia, Watoto wengi wa kike wanaolewa wakiwa na umri wa miaka 11, 12 hadi 15 na wote wanaachishwa shule.