Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Naomba radhi kwenye uzi, nitatumia majina ya viongozi ambao naamini wamefutwa kwenye ramani ya siasa si kwa kushindwa hoja, bali kwa matumizi makubwa ya mfumo uliokuwa imejichimbia kwenye shimo la uzalendo.
Tuliambiwa matajiri wataishi kama masikini, tukashangilia; huku mataifa yaliyoendelea, tajiri mwenye kipato cha halali analindwa, Tanzania, tajiri kama MO, ambaye anautajiri wa haki, aliona joto ya jiwe. Naamini ipo siku MO amewahi kujitoa kuwa tajiri, naamini amewahi kuwaza, bora angekuwa masikini, may be angepumua.
Chenge ni mwanasiasa nguli aliyejijenga kwao Bariadi, lakini iliamuliwa asiwe mbunge na hakuwa. Iliamuliwa asisikike na hakusikika, ikaamuliwa aishi maisha yasiyo na amani na ikawa hivyo.
Tuna wasomi nguli kama Prof Muhongo, huyu mwamba alichora ramani ya REA kuonyesha umuhimu wa nishati vijijini. Pamoja na unguli wake, alidhalilishwa, akalikimbia bunge kwenda kujificha nje kwa muda, alivamiwa nafsini kwa maneno makali yaliyopelekea aogope kwenda jimboni kwako na asitamke neno bungeni.
Edward Lowasa na Sumaye, pamoja na kuwa mawaziri wakuu, hila hadhi zao ziliwekwa kando; wakapokonywa kila kitu na kunyimwa haki ya kujipanua kisiasa. Ghafla, wakalazimishwa bila kutaka wasimame jukwaani wamtukuze mwamba na kumsifia.
Wabunge 19 wa Chadema, pamoja na waunga mkono juhudi za Baba, wale wanachama wanateseka sana moyoni kwa sasa. Wananyanyasika sana kuzaliwa na kipaji cha siasa, then wakalazimishwa kwa kupewa ajira na vipande wa fedha, wasaliti imani yao na waimbe wimbo wa watawala. Mdee na wenzake hawakuwa kuhitaji nguvu ya mwanaume yoyote, washinde ubunge, walikuwa wanashinda kwa hoja. Leo, future yao kwenye siasa imeharibika, wanaishi kwa hisani.
Vijana wadogo kina Nassary wameibadili itikadi kutoka itikadi hai, wakavaa itikadi mfu. Wanaishi kinyonge just kwa sababu waliambiwa wachangie moja, kuishi au kutembea.
Hawa watu na wengine, wakiwemo wafanyabiashara ambao fedha zao zilikwapuliwa kwenye mabenki, si watu wa kukaa nao kizembe; ni watu wanapaswa kurejeshewa amani iliyopotea.
Tusifanye kosa tukaamini wanaamani, wametulia wanatafuta upenyo. Siku yao au familia zao wakipata upenyo mtalia na kusaga meno. Waombeni radhi, kaeni nao kwa taadhari kwani binadamu wote wana ukichaa.
Sijui mmenielewa?