Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 259
Malengo ni kujenga uwanja wenye uwezo wa kuingiza watazamaji zaidi ya 30,000.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba kwa wakati huo, Barbara Gonzalez, ndiye aliyekuwa akizungumza zaidi siku ya uzinduzi huo akiwa sambamba na Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu.
Tangu mchakato ule umeanza hadi leo ni takribani miaka miwili, hakuna tulichoambiwa nini kinaendelea.
Mara ya mwisho niliona viongozi wa Simba wakienda kuangalia eneo la uwanja huo na kuanza mchakato wa kuzungushia uzio baada ya kuwepo kwa mvutano baina yao na majirani zao huko Bunju.
Kinachonishangaza zaidi, zile fedha zilizokuwa zinachangwa, haijatoka figure kamili ya kwamba kilipatikana kiasi gani kwa sababu mashabiki na wanachama wa Simba walikuwa wakichanga kuanzia Shilingi 1000 za Kitanzania.
Projekti ya uchangiaji ikafa kihuni bila ya kuwepo kwa maelezo, hapa ni wazi kuna upigaji umefanyika.
Sasa kama kuna viongozi wanaanzisha vitu kwa kutumia rasilimali za klabu kisha wanajaza matumbo yao, inabidi tuwe nao macho kwani hawana faida katika maendeleo ya soka letu.