Kwanza ni wape pole kwa kazi kubwa mnayoifanya ,viongozi wangu wa manispaa ya Temeke.Ninaimani kubwa na nyinyi ,hasa katika kuwaletea maendeleo wana Temeke wote.
Pili,niipongeze manispaa ya Temeke ya kujenga kituo cha mabasi kwa kata ya Buza .Kwa kweli ni jambo la maana na lakupigiwa makofi.
Tatu,ni ushauri wangu hasa juu ya STENDI MPYA YA BUZA-KWA MAMA KIBONGE/NJIA PANDA YA KITUNDA.
Stendi hii iliyopo njia panda ya kitunda uelekeo wa mwanagati Kitunda kinyantira na mbagala ,ni stendi bora na ya kuvuti.Ikiwa chini ya mwamvuli wa 'uchumi wa fremu" na tozo za magari.
Kiukweli sina shaka na stendi ila ,kinachonikera kuona kuwa ni "ukosefu wa ubunifu" .Nayo ni kuona magari yanalazimishwa yaingie katika stendi hii mpya na iwe mwisho wa ruti zote za Buza. Kwa kulazimishana huku ,hakutafikia malengo,kwani kitendo hiki kinawaumiza wanachi wakipato cha chini,kwani kinawapandishia gharama za usafiri.
Haiwezekani nilipe sh.600 toka Buza kanisani mpaka stendi mpya,alafu tena nipande gari la kwenda ,buguruni,tandika au Kariakoo kwa sh.600 tena. Yani ruti ya sh.600 nitumie sh.1200,haya ni makusudi na kuleta maumivu makubwa kwa watu.
Pia, kuna stendi iliyojengwa Buza kanisani, ambayo ilikuwa imekamilika kwa kiasi.Je, hii imekosa ubora gani?
Nani aliamua ijengwe? Kwanini isitumike? Fedha za ujenzi ni kodi zetu?
JE, MLIJENGA KWA KUJIFURAHISHA? INAUMA.
Ni pende kutoa tuu rai.
Stendi mpya iwepo,ila zianzishwe ruti mpya zinazoweza kutoka hapo Buza/Njiapanda Mvuti Chanika, Chamanzi, Tegeta,,Kibamba, Kigogo, Vikindu, Kigamboni. Kuanzishwa kwa ruti hizi ,zitafanya kituo kuwa hai,na kutokuchochea magomvi na wanachi.
Pili ruti za kanisani Buza iachwe iendelee ,kuwahudumia wanachi wanaoishi maeneo ya
Kwalulenge,Kanisani,Sigara,mpka lumo na Kipera.
Natumaini ,maoni yangu yayakufikia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke.
Asante