Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kifo cha kiongozi wa muda mrefu wa Hizbullah japo kimekuwa ni huzuni kubwa kwa wananchi wa Lebanon na wapenda haki hata hivyo hakijaleta taswira ya kumalizika mapambano kati ya Hizbullah na taifa hilo la kiyahudi.
Muda mfupi tu baada ya kutolewa uthibitisho wa kifo cha kiongozi huyo kombora zito limerushwa katikati ya Jerusalem na kusababisha moto mkubwa bila kutolewa takwimu zaidi za hasara iliyopatikana.
Kwa upande wao wapiganaji wa Houth nao wamerusha makombora mawili moja kuelekea TelAviv na moja kuelekea meli za kivita za Marekani kwenye bahari ya Yemen na bahari nyekundu.Yote hayo yanathibitisha kuwa vita kati ya Israel na maadui zake wa mashariki ya kati havitasimama kutokana na kuuliwa au kufa kwa viongozi wa wa makundi hayo.
Nchini Marekni,bila haya wala kuona vibaya viongozi wa nchi hiyo akiwemo mgombea uraisi kupitia chama cha Democratic wameisifia Israel kwa kuweza kumuua kingozi huyo sawa na walivyosifia kuuliwa kwa kiongozi wa Hamas takriban miezi miwili iliyopita.