Viongozi wa mataifa ya Magharibi na taasisi za Kimataifa wamekemea vikali mashambulizi dhidi ya Ukraine na kuahidi kuiwajibisha Urusi

Viongozi wa mataifa ya Magharibi na taasisi za Kimataifa wamekemea vikali mashambulizi dhidi ya Ukraine na kuahidi kuiwajibisha Urusi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Viongozi wa mataifa ya Magharibi na taasisi za Kimataifa wamekemea vikali mashambulizi dhidi ya Ukraine na kuahidi kuiwajibisha Urusi.

Mara baada ya kuripotiwa taarifa ya milipuko katika miji mbalimbali ya Ukraine, Rais wa Marekani Joe amemshutumu Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kusema “Urusi pekee itawajibika kwa vifo na uharibifu utakaotakana na mashambulizi, Marekani na washirika watajibu kwa njia stahiki, dunia itaiwajibisha Urusi”.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema “Nimeshtushwa na matukio ya kuogofya Ukraine na nimeongea na Rais Zelenskyy kujadili hatua inayofuata. Rais Putin amechagua njia ya umwagaji damu na uharibifu kwa kuanzisha mashambulizi ya uchokozi dhidi ya Ukraine. Uingereza na washirika wake tutajibu mapigo kikamilifu”.

Rais wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen kwa upande wake amesema “Tunakemea vikali mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine. Katika nyakati hizi, tuko pamoja na Ukraine na wanawake, wanaume na watoto wasio na hatia wakati wakikabiliana na mashambulizi haya ya kichokozi na hofu dhidi ya maisha yao. Tutaiwajibisha Kremlin”.

Nae Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema “kwa hali inayoendelea nabadili ombi langu, Rais Putin, kwa wito wa ubinadamu, rudisha vikosi vyako Urusi. Mgogoro umalizike sasa”.

Usiku wa kuamkia leo, Urusi ilianza mashambulizi makubwa dhidi ya Ukraine, huku milipuko ikiripotiwa katika miji mingi na nje ya maeneo yenye machafuko ya mashariki yanayoshikiliwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.
 
Ingawaje siikubali Marekani na washirika wake ila anachofanya Urusi ni mambo ya karne zilizopita.

Hivi itakuwaje kama mataifa mengine yataamua kuingilia vita hii? Urusi haoni atajitengenezea mazingira mabaya ya kiuchumi maana mataifa ya ulaya yana mbinu nyingi.

Huenda yamefanya hivyo ili Urusi aingie kichwa kichwa kutumia gharama kubwa za kivita na huku ana vikwazo kila kona mwishowe anajikuta mufilisi uchumi ukiwa chali.
 
Ingawaje siikubali Marekani na washirika wake ila anachofanya Urusi ni mambo ya karne zilizopita...
Anachokifanya URUSI huko UKRAINE ni cha Kukemea kwa Nguvu Zote.

Vladimir Putin ni Hitler wa Modern Politics, Nasimama na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, NATO na Wengine Kupinga Vikali hatua za Urusi Kuivamia UKRAINE.

Poleni sana watu wa Ukraine, Mungu awalinde muwe salama.
 
Marekani ameshasema hatapeleka jeshi kuisaidia Ukraine maana Ukraine hakua mwanachama wa NATO. msaada anaoweza kutoa ni silaha tuu.

Russia kashasema anasubiri kuona pua itakayoingia mstari wa mbele kuisaidia Ukraine. Hypersonic missile zipo 100% alert kwa kazi hiyo
 
Ingawaje siikubali Marekani na washirika wake ila anachofanya Urusi ni mambo ya karne zilizopita...
Hao Marekani na washirika wake swagga na grandiosy tu ndo wanamiliki.

Putin kafanya yake utaona kama watasogeza pua.
 
Marekani ameshasema hatapeleka jeshi kuisaidia Ukraine maana Ukraine hakua mwanachama wa NATO. msaada anaoweza kutoa ni silaha tuu.

Russia kashasema anasubiri kuona pua itakayoingia mstari wa mbele kuisaidia Ukraine. Hypersonic missile zipo 100% alert kwa kazi hiyo
Kwa akili yako unazani kwa dunia ya saivi uta tumia izo silaha wakuangalie tu
 
Rusia kasema nchi yoyote itayoingi vitan kuisaidia Ukraine Hypersonic missile zipo standby 100% kwa ajili yake....means ukiingia kuisaidia ukraine unapigwa nyumban kwako..
 
IMG_20220302_134803_053.jpg
In Lisichansk (LPR) there were strikes on the city tower.
 
Ukrainian ZRPK "Tunguska" in the Nikolaev region.
 
The story of how the Ukrainian media continue to attach "Z" to Ukrainian equipment, passing it off as captured

Source: watch_media
 
A man from Bashkiria smashed an iPad with a hammer to show that he was not afraid of sanctions.

Source: Dvach
 
Back
Top Bottom