Viongozi wa SADC wasalimu amri wa Kagame! Wakubali kuondoa vikosi vyao CONGO DRC. Huu ni ushindi kwa Kagame na hatari kwa mataifa yanayomzunguka

Viongozi wa SADC wasalimu amri wa Kagame! Wakubali kuondoa vikosi vyao CONGO DRC. Huu ni ushindi kwa Kagame na hatari kwa mataifa yanayomzunguka

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Haya sasa!

SADC wamesalimu amri kwa M23/ Rwanda. Wakuu wa nchi wameamua Vikosi vilivyopo Congo viondoke.

Sote tunakumbuka, hili lilikuwa takwa na agizo la M23 na Kagame kuwa vikosi vyote vya kigeni viondoke Mashariki mwa Congo DRC.

Nadhani kwa haya yaliyotokea, sote sasa tunajua mbabe wa Afrika ni Kagame/ Rwanda!

Msiniulize tena kwa nini nitailani milele CCM kwa kutufikisha hapa.

Screenshot_20250313_181019_LinkedIn.jpg
Screenshot_20250313_181134_LinkedIn.jpg
Screenshot_20250313_181134_LinkedIn.jpg


===
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) imeamua kumaliza rasmi operesheni yake ya kijeshi katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kufuatia hasara kubwa zilizopatikana, ikiwemo vifo vya zaidi ya wanajeshi kumi na wanne mnamo Januari.


Uamuzi huu ulifikiwa katika mkutano wa kilele wa mtandaoni siku ya Alhamisi, ukihitimisha operesheni ambayo ililenga kurejesha amani na usalama katika eneo hilo ambalo limekuwa likikumbwa na migogoro kwa takriban miongo mitatu.

Taarifa ya mkutano huo wa Machi 13, 2025, ilithibitisha kuwa mamlaka ya SADC Mission in the DRC (SAMIDRC) yamekamilika, na kwamba kuondolewa kwa vikosi kutafanyika kwa awamu.

SAMIDRC, ambayo ilihusisha wanajeshi kutoka Malawi, Tanzania, na Afrika Kusini, ilitumwa DRC mnamo Desemba 2023 kusaidia serikali ya nchi hiyo kupambana na ghasia zinazoendelea.

Hata hivyo, operesheni hiyo ilikumbwa na hasara kubwa, hasa kwa Afrika Kusini, ambayo ilipoteza wanajeshi 14 mnamo Januari wakati wa mapigano. Aidha, wanajeshi watatu wa Malawi na wanajeshi wawili wa Tanzania pia waliuawa kwenye mapambano hayo.

Afrika Kusini, ambayo inadaiwa kuwa na idadi kubwa ya wanajeshi waliotumwa DRC, imekuwa ikishinikizwa kuondoa vikosi vyake, hasa baada ya ripoti kuonyesha kuwa baadhi ya wanajeshi wake wamezuiliwa kambini na wapiganaji wa M23.

Tangazo la kuondolewa kwa vikosi vya kijeshi limetolewa siku moja tu baada ya Angola kuthibitisha kuwa mazungumzo ya amani kati ya DRC na kundi la waasi la M23 yataanza wiki ijayo jijini Luanda.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema kuwa kuondolewa kwa vikosi kutafanyika kwa utaratibu, kulingana na hali ya usalama inavyoendelea katika eneo hilo.

Licha ya hali tete, alieleza matumaini kuwa juhudi za amani zinazoendelea na mazungumzo yanayotarajiwa kuanza zitasaidia kuimarisha utulivu katika eneo hilo.

SADC, kwa kushirikiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), imekuwa ikitoa msukumo kwa suluhisho la kidiplomasia na kisiasa kuhusu mgogoro huo, huku ikihimiza jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua dhidi ya janga kubwa la kibinadamu linaloendelea.

Hali inaendelea kuwa nyeti, huku kundi la waasi la M23, linalodaiwa kupata msaada kutoka Rwanda, likizidi kusonga mbele katika eneo lenye utajiri wa madini mashariki mwa DRC.

Rais wa Angola João Lourenço pia amekuwa mstari wa mbele katika juhudi za upatanishi, ambazo zimepata msukumo mpya baada ya kukutana na Rais wa DRC Félix Tshisekedi, ambaye hapo awali alikuwa akipinga mazungumzo ya moja kwa moja na M23.

Source: News Central
 
Safi sana maana hela za Umoja wa Mataifa na za SADC zulitumika vibaya kwa manufaa ya mabeberu wa Marekani ya Kaskazini, Ulaya na China wachimbe madini Kongo.


12 March 2025

A message to President Tshisekedi | Aid | Rwanda's Dignity | President Kagame talks to Mario Nawfal

Walitaka nchi ya Rwanda iwe tupu watu wakimbie, tunakumbuka mamilioni ya waNyarwanda waliwahi kukimbilia Tanzania, Congo na Uganda


View: https://m.youtube.com/watch?v=IvXf5JgmIxs

Inaonesha jeshi la serikali ya Kongo FARDC na mgambo wa FDLR walikuwa wamejipanga kuivamia Rwanda kutokana na mpangilio wa zana zilivyopangwa (formation) kuelekea nchi ya Rwanda. Mhariri mtendaji James Munyaneza anasimulia kwa undani hali hiyo alivyokuwa amejipanga Tshisekedi ..

Misaada ya kimataifa inatumika na mataifa makubwa kama silaha ya kivita (Aid as a weapon tool), kuburuza nchi za kiafrika ... kutaka zifanye mambo nchi beberu zinataka ...

Mheshimiwa rais Kagame una ujumbe gani kumwambia rais Felix Tshisekedi ?

Kwa kweli ninamhurumia Felix Tshisekedi kwa kuwa rais wa Kongo, ajibu mheshimiwa Kagame baada ya kuulizwa swali hilo gumu kutokana na hali iliyopo sasa eneo hilo la nchi za Maziwa Makuu..

UN kwa miaka 24 iliyopita, imetumia US$ 40 bilioni kugharamia majeshi ya kulinda amani Congo kutoka Latin Amerika, Bara Asia na wale wa kutoka bara Afrika, hiki ni kiasi kikubwa cha 'misaada' lakini hakuna Amani Congo, tujiulize ki kwanini..

Amani nchini Kongo itapatikana tu kama serikali ya Kinshasa ya Tshisekedi watakubali kukaa katika meza moja na kundi la M23 kuzungumzia, hapo amani ndiyo itapatikana asema Rais Kagame akijibu swali la Mario Nawfal blogger mwandishi wa kiMarekani..

Pia Kongo isisahau umuhimu wa usalama wa Rwanda, kwa kukidhibiti kikundi cha mgambo wa Intarahamwe cha FDLR, ...
 
ote sasa tunajua mbabe wa Afrika ni Kagame/ Rwanda!
Tumia akili kidogo na ujaribu kupunguza mhemko!

8 Mar, 2025 19:36

considering-minerals-deal/

Is Trump mulling a minerals deal with conflict-hit DR Congo?​


 
Tumia akili kidogo na ujaribu kupunguza mhemko!

8 Mar, 2025 19:36

considering-minerals-deal/

Is Trump mulling a minerals deal with conflict-hit DR Congo?​


Nyie endeleeni tu kuimba mapambio ya CCM mitano tena na kujenga Bar kwenye kambi za Jeshi.

Badala ya ku invest kwenye majeshi yenu na intelligence mnawekeza kwenye machawa.

Na bado. Alivyo mshenzi yule Mr. Slim atawapumulia hadi visogoni.
 
Huyo Rais wa Congo nadhani kama hajawapa basi yupo mbioni kuwapa USA mali zote on a silver platter (ni yale yale kama walivyomtumia Mobutu kama puppet wao); Ila ndio hivyo waafrika tunatafutana uchawi wenyewe kwa wenyewe wakati watu wanafaidi huko mbali..., Divide and Rule bado na itaendelea kututafuna mpaka keshokutwa..

And an average Congolese continue to suffer (minerals kwake zimekuwa a curse)
 
Inabidi ukubali matokeo.

Huwezi beba mzigo ambao aubebeki

Swala ni kuimarisha ulinzi wetu.

Uhalisia ni kwamba serikali ya Congo aijawahi kuwa na full control ya eneo lake.

Sio East Congo tu, tuwaache nchi ijimege yenyewe mpaka kila eneo liwe na serikali yake.

Kama vipi wazungu waingilie kati.

Cha msingi JWTZ kipindi hiki cha upuuzi unaoendelea Congo, mipaka ya Tanzania sio ya kuchezea.

We have played our part kwenye kuilinda, Congo but not sustainable.

Sasa wasijaribu Tanzania atutakuwa na msalie mtume na watanzania wenzetu wasio na loyalty na ardhi yetu.

Wasaliti tutawapeleka huko wanapokuita nyumbani kwao huku wamelala kwenye matoroli (watalazwa vipi kwenye matorili watajua muda ukifika wakileta usaliti).

Ujinga wafanye huko-huko Tanzania ni nchi isiyo na udini, ukabila wala ubaguzi wa rangi. Lakini usaliti kwa Tanzania atutovumilia.
 
Inabidi ukubali matokeo.

Huwezi beba mzigo ambao aubebeki

Swala ni kuimarisha ulinzi wetu.

Uhalisia ni kwamba serikali ya Congo aijawahi kuwa na full control ya eneo lake.

Sio East Congo tu, tuwaache nchi ijimege yenyewe mpaka kila eneo liwe na serikali yake.

Kama vipi wazungu waingilie kati.

Cha msingi JWTZ kipindi hiki cha upuuzi unaoendelea Congo, mipaka ya Tanzania sio ya kuchezea.

We have played our part kwenye kuilinda, Congo but not sustainable.

Sasa wasijaribu Tanzania atutakuwa na msalie mtume na watanzania wenzetu wasio na loyalty na ardhi yetu.

Wasaliti tutawapeleka huko wanapokuita nyumbani kwao huku wamelala kwenye matoroli (watalazwa vipi kwenye matorili watajua muda ukifika wakileta usaliti).

Ujinga wafanye huko-huko Tanzania ni nchi isiyo na udini, ukabila wala ubaguzi wa rangi. Lakini usaliti kwa Tanzania atutovumilia.
Unawatisha wakati Jeshi lako saivi limekuwa Jeshi la siasa na kupiga picha.

Hao TISS ndo wanashindana kujipendekeza kwa CCM kuwaibia hadi kwenye chaguzi za vijiji.
 
Unawatisha wakati Jeshi lako saivi limekuwa Jeshi la siasa na kupiga picha.

Hao TISS ndo wanashindana kujipendekeza kwa CCM.
Kama kuna watu wanajiona sio watanzania huu ndio muda wa kwenda wa kuchagua nchi wanayotaka.

Kama kwenda kuipigania East Congo, Rwanda, Burundi na kadhalika,

Mimi siafikl serikali ya Tanzania kujiingiza katika hiyo, migogoro; Iła kama upande wako sio Tanzania akutakuwa na mwamwana kwenye usaliti wa Tanzania.
 
Hakuna manufaa yeyote kwa SADC kuwepo eastern congo. Ni kujiongezea gharama zisizo na msingi. Kagame hajapata ushindi wowote maana mapigano yanaendelea. Suluhu ya matatizo haya ni kuongea kati ya serikali ya congo na kundi la M23 . Nimefurahi kusikia Tshisekedi amekubali kukutana na M23 katika mazungumzo yaliyoitishwa na Angola.

Msipende kushabikia vita athari ni kubwa kuliko faida .
 
Back
Top Bottom