Viongozi wa Serikali siyo wazazi wetu bali ni watumishi wa umma

Viongozi wa Serikali siyo wazazi wetu bali ni watumishi wa umma

Izia maji

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
2,997
Reaction score
5,385
Nimeona clip ya Nape Nauye akifoka na kumwambia Tundu Lissu amuheshimu Rais Samia kwa kuwa ni mama yake. Sawa hatukatai kuwa kila mtu anastahili heshima na si viongozi tu wa serikali na kisiasa.

Kosa kubwa ni pale machawa wa viongozi wanataka chawa wao wasikosolewe wala kofokewa wanapofanya mambo ya hovyo katika jamii. Wanawataka wakosoaji watumie maneno ya staha kufikisha ujumbe!

Huu ni upuuzi kwa sababu hakuna staha kwa mpuuzi na lazima akabiliwe kulingana na upuuzi wake. Viongozi siyo wazazi wetu bali ni watumishi wetu na wanapaswa kutenda majukumu yao kwa mujibu wa sheria. Haiwezekani watu wauze rasilimali za Taifa halafu wategemee staha kuwakabili. Kwa vyo vyote vile wategemee kukabiliana na lugha yo yote ile ikiwemo lugha chafu kulingana na uchafu wao!

Nafasi walizonazo serikalini na kisiasa ni mali ya umma na kama hawaziwezi waondoke haraka, kuna mamilioni ya wananchi wenye uwezo wa kushika nafasi zao tena kwa ufanisi mkubwa zaidi! Wengi wa viongozi waliopo wamepata nafasi hizo kwa kurithishana na si kwa uwezo wa kiutendaji! Na ili waendelee kubaki katika nafasi hizo wanatumia kila aina ya vitisho kuzuia wengine!
 
Mzazi siyo lazima awe ni yule aliyekuzaa

Ndio sisi Wengine tulimkemea Makonda alivyomzongazonga mzee wetu Warioba wakati wa kutafuta Katiba mpya

Tukamkemea na kibabu Sadifa alivyomtukana Mzee Lowassa!
 
Mzazi siyo lazima awe ni yule aliyekuzaa

Ndio sisi Wengine tulimkemea Makonda alivyomzongazonga mzee wetu Warioba wakati wa kutafuta Katiba mpya

Tukamkemea na kibabu Sadifa alivyomtukana Mzee Lowassa!
Acha nahau za kijinga!
 
Back
Top Bottom