Viongozi wa Serikali watakiwa kuwasilisha taarifa za Mali na Madeni kabla ya Desemba 31, 2024

Viongozi wa Serikali watakiwa kuwasilisha taarifa za Mali na Madeni kabla ya Desemba 31, 2024

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Kamishna wa Maadili, Jaji (Stahiki) Sivangilwa Mwangesi amewakumbusha na kuwataka viongozi wote wa umma wanaotajwa kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kuwasilisha tamko la rasilimali na madeni yao kabla ya Desemba 31, 2024.

Amesema hayo leo katika taarifa yake kwa umma iliyochapishwa kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa sekretarieti ya maadili ya umma na kuongeza kuwa, hatua hiyo inalenga kuhakikisha uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali za umma, sambamba na kukuza imani ya wananchi kwa viongozi wao.

Katika taarifa yake, Kamishna Mwangesi amesisitiza umuhimu wa kuzingatia masharti ya Ibara ya 132(5)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na kwamba utekelezaji wa takwa hili ni sehemu muhimu ya kulinda maadili ya uongozi wa umma.

Tamko la Rasilimali na Madeni linatoa taswira ya uadilifu wa kiongozi katika utumishi wa umma na linapaswa kuwa halisi na lenye taarifa sahihi, likijumuisha mali zote pamoja na madeni yanayowahusu moja kwa moja.
 

Kamishna wa Maadili Jaji (Stahiki) Sivangilwa Mwangesi anawakumnusha viongozi wote wa umma waliotajwa kwa mujibu wa Sheria kuzingatia takwa la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 Ibara ya 132(5)(b) kuwasilisha Tamko la Rasilimali na Madeni kabla ya tarehe 31.12.2024.
 
Back
Top Bottom