KERO Viongozi wa Serikali za Mtaa Skanska Mashimoni, mnatarajia tuwachague tena mwaka huu kwa mazingira haya?

KERO Viongozi wa Serikali za Mtaa Skanska Mashimoni, mnatarajia tuwachague tena mwaka huu kwa mazingira haya?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
1724230799737.png

Kituo cha Skanska maeneo ya Barabara ya Bagamoyo kuanzia mtaa wa Mashimoni hadi kuelekea Mtongani, hali ya mazingira ni mbaya mno, na afya za wananchi ziko hatarini.

1724230583050.png

Mifumo ya maji ni mibovu, japokuwa hiki ni kipindi cha jua kali bado madimbwi ya maji machafu yamejaa kila kona. Najiuliza kwa hali Tanzania tutaweza kweli kumalizana na Kipindupindu na Malaria.

1724230623711.png
Kingine hakuna utaratibu mzuri wa utapaji taka. Sijawahi kuna magari ya taka yanapita sehemu hiyo kukusanya taka. Yaani taka zimezaa kila mahali. Kila baada ya wiki mbili watu wa taka wanapita kukusanya taka majumbani na tunawalipa lakini cha kushangaza ni kwamba taka hizo wanaenda kumwaga pembezoni mwa bararaba mitaani kwenye makazi ya watu. Yaani mitaa ni michafu hadi kero


1724230683254.png
Miundombinu ya barabara ni mibovu. Kwanza bolt zinagoma kufika katika maeneo hayo kwa sababu ya ubovu wa barabara hiyo. Mtu ukipata dharura ya ugonjwa ni ngumu kupata usafiri isipokuwa bodaboda. Kipindi cha mvua ndo balaa linapokuja sasa maji yanajaa barabarani kupita ni ngumu sisi watu wa makazini tunashindwa kwenda kazini na wanafunzi wanalazimika kubaki nyumbani wasiende shule.
1724230740258.png
Najiuliza hivi viongozi ni kwamba hawaoni suala hili au wameamua kulifumbia macho kwa sababu hii ni kero kwa wananchi. Viongozi hawa wanategemea tuwapigia tena kura Novemba kweli?
 
Jukumu la kutunza mazingira na kuyalinda ni la jamii nzima. Anza wewe Kisha wengine wafate ili ikibidi hata uchukue nafasi ya hao viongozi siku za usoni. Mwafrika wa Sasa na mazingira ni paka na panya pakiwa pazuri atakuja hata usiku mnene apaharibu ili mradi nafsi yake ifurahi.
 
Miaka ya 2017-2019 nikiwa naishi maeneo ya Mtongani niliwahi kupita hayo maeneo na kujiuliza maswali mengi sana. Inakuwaje huko mashimoni hakuna mpangilio mzuri wa miundombinu na makazi? Na je serikali ilifikiria nini kuruhusu hayo yatokee?
Kwa hiyo hayo yanayotokea sasa hivi ni matokeo ya ujenzi holela wa makazi bila kuzingatia mpangilio wa miundombinu hasa barabara.
 
Back
Top Bottom