Viongozi wa Simba acheni usanii juu ya suala la kipa wenu

Viongozi wa Simba acheni usanii juu ya suala la kipa wenu

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Napata shida kubwa juu ya tetesi zinazoendelea ya kwamba simba inaweza kumtema kipa mbrazil aliyesajiliwa hivi karibuni kwa sababu eti ana majeraha!!!
Siwezi kusema Sana juu ya tetesi inawezekana ikatokea kweli ama isitokee, lakini Kama ni kweli basi kuna wahuni wanaendelea kupiga 10% kwa wachezaji wanaosajiliwa
Kwa akili ya kawaida kinachoanza kati ya hivi viwili ni kipi; a) kumfanyia vipimo mchezaji kwanza ndio umsainishe mkataba au b) unamsainisha mkataba kwanza ndio unamfanyia vipimo?
Najua viongozi wa simba ni wasomi na waelewa wa mambo lakini waliruhusu vipi kikatokea kitu kama hiki?
Mchezaji na wakala washavuta mpunga wao, unaenda pia kuvunja mkataba wa miaka 2 ambao aujamaliza ata wiki 2 unalipa tena mamilioni!!!!?????
Napata tabu kama itakuwa ivyo, bado nawaza kwamba sababu sio iyo bali ni uwezo mdogo wa kipa husika na kutokidhi vigezo vya TFF juu ya wachezaji wa kigeni, suala la majeraha linawekwa ili kufunika uozo wa kutokuwa makini kwenye kumsajili,
Na penyewe kuna maswali mengi yasiyokuwa na majibu, mpaka wanamsajili awakumfuatilia ligi aliyokuwa anacheza? Mpaka wanamsainisha mkataba awakujua sheria na kanuni zilizowekwa na tff juu ya mchezaji wa kigeni? Je lilikuwa ni pendekezo la robertinho au la viongozi?
Bidhaa za kununua online mara nyingi uwa zina shida!
 
Iundwe tume ya uchunguzi kubaini huo upigaji uliojitokeza mwenyekiti awe mo
 
Simba ni SIKIO la kufa.

Nilimtumia Email KAJULA.

Nilimuonya kutosajili wachezaji Nje ya Africa.
Nikaambatanisha na mifano.

1. Dejan.
2. Santos.
3. Wilker Da silver.
4. Falager.

Lakini wapi.
LEO AIBU IMEWAPATA
 
Simba ni SIKIO la kufa.

Nilimtumia Email KAJULA.

Nilimuonya kutosajili wachezaji Nje ya Africa.
Nikaambatanisha na mifano.

1. Dejan.
2. Santos.
3. Wilker Da silver.
4. Falager.

Lakini wapi.
LEO AIBU IMEWAPATA
Mjiandae kumlipa Miquison pia maana mtavunja tu mkataba wake, tena mmejifunga miaka mitatu.

Biashara ya ten percent Simba imeota mizizi.
 
Back
Top Bottom