Viongozi wa Simba ndio wanaiua timu bila wao kujua kwa kufanya usajili wa kizamani mwishowe wanapoteza wachezaji je nini kifanyike?

Viongozi wa Simba ndio wanaiua timu bila wao kujua kwa kufanya usajili wa kizamani mwishowe wanapoteza wachezaji je nini kifanyike?

Sasa huoni kama ilo litawapotezea ata ayo maslahi wanayopata endapo mashabiki na wanachama watachukua hatua dhabiti juu ya klabu ?
Hahahahaha mashabiki nyie wa mpira wa simba na yanga si nyie ndio ccm, huwa mnachukuaga hatua kweli? Mpk siku mnachukua hatua wao si wameshiba vya kutosha ?
 
Tatizo LA simba ni mashabiki
Mfano wa humu jamvini nadhani unawajua e.g GENTAMYCINE
Wamefanya nini na hoja yako ni ipi ? Nafikiri baadhi yao kama Genta wamechagua namna yao ya kuipambania club yao kwa njia tofauti ambayo inaweza kuwa ya ajabu kwa baadhi yenu ila kwake ndio silaha kuu inaleta maana
 
Ndiyo safi mafuvu yataanza kufanya kazi, binadamu akipata changamoto huamsha ubongo
Nakubaliana na wewe labda hili litawazindua. Tangu mwanzo tukisema kama uvunjaji wa mkataba ni rahisi kama alivyofanya Awesu basi Hakuna haja ya Mikataba.
 
Kumbe kauli mbiu ya nguvu moja haiwezi kutekelezeka kwenye jamii mfu,(silent society), jamii ambayo haiwezi kuhoji kila jambo ndiyo bwana. Simba sc ni mfano hai kwa jamii yetu ambayo haiwezi kuhoji
 
Kwa sasa ni kazi sana kutetea mambo ya Simba. Pale hakuna viongozi ni mafuvu tu
Wanachama je? Chanzo kikuu ni wanachama ambao hawezi kuhoji viongozi na muwekezaja labda kwa vile asilimia 51 haina nguvu na hilo ndilo tatizo lenyewe, swali fikirishi kwanini asilimia 51 haina nguvu, (majibu), jibu litakalo patikana ndiyo suluhisho la simba sc
 
Nakubaliana na wewe labda hili litawazindua. Tangu mwanzo tukisema kama uvunjaji wa mkataba ni rahisi kama alivyofanya Awesu basi Hakuna haja ya Mikataba.
Ili suala mikataba pia TFF isipoangalia usimba na uyanga basi litakuja leta maafa
 
Back
Top Bottom