Hivi mchango wa familia ya Dewji pale Simba mnaichukulia poa siyo?
Labda niwakumbusheni...
Wakati Simba inafanikiwa kufika hatua ya fainali ya michuano ya CAF mwaka 1993,mfadhili alikuwa ni AZIM DEWJI. Kabla hajaingia Simba nadhani mlikuwa hamjawahi kucheza fainali tangu timu ianzishwe.
Wakati Simba inaingia makundi ya Champions League kwa kuitoa Zamalek ya Misri,mwaka 2003,mfadhili alikuwa ni MO DEWJI (kupitia MeTL). Ni miaka mingi sana ilikuwa imepita tangu mlipofikia hatua hii mara ya mwisho kabla MO hajazama kuifadhili Simba.
Ni MO DEWJI tena ndo alieiwezesha Simba kuvuka hatua ya makundi na kuingia robo fainali,kwenye Champions League msimu wa 2018/2019.
Sasa sijui hao akina Hamis 'Mhogo mchungu' Kigwangala, Mzee Kilomini, na wenzao wa calibre yao sijui walikuwa wapi kuipa Simba mafanikio hayo?
Sasa nyie Simba jichanganyeni muone.