Viongozi wa Simba wanawalipa wachambuzi ili wamchafue Fabrice Ngoma"

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Viongozi wa Simba wanawalipa wachambuzi ili wamchafue Fabrice Ngoma"

Fausty Mkandila, wakala wa Fabrice Ngoma.

Maoni yangu : hili linawezekana kwa asilimia mia kama waliweza kumlipa Mgana Mickyjnr ili amchafue Azizi ki watashindwa hili?!

Aziz ki sahivi Yupo moto anauwasha Kila kukicha Huyo Micky jnr anajifanya haoni kama ni mwandishi alipaswa Kuandika Positive na Negative kumuhusu Azizi ki na siyo kuegamia Upande mmoja.

Naungana na wakala wa Fabrice Ngoma wachambuzi wanalipwa ili wampe presha aonekane hafai akae mbao Ndefu asicheze kabisa.
 

Attachments

  • 20240812_112549.jpg
    147.5 KB · Views: 5
acha ubishi wa kitoto ukweli ni kwamba fabrice ngoma kwa sasa ameisha na si yule wa kipindi cha nyuma. aachwe tu
 
Vitu vingine hata havihitaji elimu ya ziada, Ngoma sasa hivi AKILI na MWILI vinapishana maamuzi.. Ndo maana mechi na Coastal Union kadi zote alizopata ni kwa sababu ya kushidwa kasi.

Ngoma umri umeshaenda, hakuna cha mtu kulipwa ni ukweli ulio wazi...

Ngoma, Mzamiru na Kibu kwa sasa ni ABIRIA tu Simba hakuna MSAFIRI hapo...

MUTALE ni new-SAIDO halafu MUKWALA ni 95% ya JOBE... TUENDELEE NA UVUMILIVU WA HALI NA UKWELI ULIOPO TUKIENDELEA KUIJENGA TIMU....
 
umemaliza kila kitu ndugu na nadhani baada ya hii post yako tu basi na hata huu uzi nao ufungwe ili tusipotezeane muda
 
Mara mia Babu Saido angebaki aiseee
 
unasema? yaani yule mchezaji waliyemuiba eapoti,ndio wanamsema?
 
MMEANZA KUMKATAA MUTALE
 
😂😂 Mbona vilio vimeanza mapema sana
 
NAISHUKURU TEAM YANGU YA YANGA HAIKUMCHUKUA HUYU JAMAA!HONGERA ENG HERSI UNAJUA KUTAMBUA WACHEZAJI BORA
 
Umemsahau kapombe
 
Itoshe tu kusema wewe ni utopolo pro max,mpira mchezo wa wazi sio kama ngono kufanywa gizani,umifloopy unaonekana tu
 
Yanga kutwa wanamtukana Micky Jr si viongozi si mashabiki unataka awaandike ili iweje kwa mfano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…