Viongozi wa Tanzania mnafahamu kwamba wanaotukopesha (matajiri) wanafanya kazi saa ishirini na nne? Sisi tunakwama wapi kuruhusu biashara 24hrs?

Viongozi wa Tanzania mnafahamu kwamba wanaotukopesha (matajiri) wanafanya kazi saa ishirini na nne? Sisi tunakwama wapi kuruhusu biashara 24hrs?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Jeshi la Polisi wanapiga marufuku wanafanya biashara ya usafirishaji abiria kufanya kazi masaa ishirini na nne lakini wao wapo kazini masaa ishirini na nne wanamlinda nani?Kwanini tumekariri kwamba tunapaswa kuwa na mfumo wa kufanya kazi Mchana pekee?

Kwanini Polisi wasisimamie usalama wa vyombo vya usafiri usiku? Hii ni nchi huru tunawaogopa majambazi? Je Mchana hakuna wizi?

Viongozi tafakarini, nimeona Tanga, Kilimanjaro na Arusha Mwisho wa safari za abiria ni saa Sita usiku wakati upo uwezekano kabisa wa aboria kusafiri 24hrs, mbona magari hayo hayo hakuna anayekataza kusafiri usiku ikiwa yamekodiwa kwenye majanga mfano msiba? Let us rethink

Soko la karikoo linafanya kazi masaa 14 hadi 16, kwanini wasifanye 24hrs? Tunashindwa kufungua taa na kuimarisha ulinzi wa taasisi za kifedha? Tunatambua kwamba wapo wafanyabiashara wangependa kununua vitu usiku na kusafiri mchana au kununua mchana na kusafiri usiku? Tutawezaje kulipa madeni kama tutaendelea kuishi na fikra za kulala saa kumi na mbili?

Stend ya mabasi mbezi Luisi inafanya kazi mchana tu, kwanini stend kama Ile isiwekewe miundombinu na kutangazwa kufanya kazi 24hrs?

Bar nyingi zinafungwa saa Sita na ukichelewa Polisi wanatinga kuwafurusha au kuwafungia Ndani? Kwanini tusiache biashara watu wajipangie muda wa kufunga na kufungua na kuondokana na mifumo inayohalalisha jambo lililokatazwa Kwa rushwa? Bar tunajua zinafanya kazi 24 hrs na watu wanapewa mpunga kimtindo; kwanini tusiruhusu Hawa walipa Kodi wakala jasho la bila kizingiti?

Mabenki yanafungwa saa kumi, nani kawaambia Mwisho wa kutoa na kuweka fedha ni saa kumi?Hizi mentality za kikoloni tunazitoa wapi?

Najiuliza maswali haya baada ya kuona kwamba wanaotukopesha wanafanya kazi masaa 24 lakini sisi tunafanya kazi masaa nane kisha muda uliobaki tunapumzika. Maana yake sisi tunaraha kuliko wale wanaotukopesha? Lini tutabadilika na kwenda na Kasi ya Dunia?

Ni Lini tutapata watawala wanaoona opportunity kwenye ulimwengu wa kutoa huduma masaa ishirini na nne?

Tumefika mahali hata wagonjwa nao tumeamini wanapaswa kuugua mchana tu, hospitali nyingi usiku zimebaiki na manes na nyingi kufungwa; tumewahi jiuiza tumesababisha vifo vingapi kwa mfumo huu wa kuruhusu huduma mchana pekee nausiku kuona kama ni muda wakulala?Lini tutaona fursa ya kufanya kazi masaa 24 kama njia ya kupunguza tatizo la ajira?

Tunapaswa kuishi Kwa kuangalia matakwa ya wengi siyo wachache
 
Masaa ishirini na nane ni tofauti na Masaa 24. Ishi humo.

Anyway: You got the point.
 
Uwiano wa idadi ya polisi na wananchi kwa ulaya na Afrika upoje? Tuanzie hapo kwanza.
 
Umewaza vyema kiongozi,bado tuna viongozi wanaowaza kijima sanaa katika Karne hii mpya.

Mfano mdogo Tu,mwaka huu kuna changamoto kubwa sanaa ya mvua,wakulima wengi hawatafanikiwa kupata mavuno ya kutosha. Lakini ukiangalia nchi inayo ardhi nzuri kubwa na yenye rutuba,tuna vyanzo bingo sanaa vya maji visivyokauka mwaka mzima.

Nashangaa wizara ya kilimo inashindwa nini kuandaa mashamba darasa na kufyeka mapori,ili vijana hawa wasio na ajira huku mtaani wakaingia shambani na kupewa zana bora kwaajili ya kufanikisha hilo.

Ukiangalia hawa ma bwana shamba nchini ni weengi lakini hakuna kazi wanafanya zaidi ya kulipwa mshahara wa bure.

Nchi kama Egypt imeendelea kupitia kilimo cha umwagiliaji,na kinaingizia nchi pato kubwa sanaa.
Ifike hatua viongozi wetu waache kuishi kwa mazoea,waumize vichwaa.

Magu alijitahidi sanaa kuondoa sherehe zilizokuwa zinaigarimu nchi fedha nyingi,na kuamishia fedha hizo kwenye miradi ya maendeleo(na kwa takwimu Tanzania ni moja ya nchi ambayo, serikali ina matumizi makubwa sanaa ya pesa za uendeshaji,naona hata vile vikao vya wizara visivyo na tija zaidi ya upigaji vimerudi kwa Kasi ya kimbunga),tujifunze hata hili dogo tu kwake,hakika tutapiga hatua.
Matumizi mabaya ya fedha ni chanzo cha umasikini.
 
Jeshi la Polisi wanapiga marufuku wanafanya biashara ya usafirishaji abiria kufanya kazi masaa ishirini na nne lakini wao wapo kazini masaa ishirini na nne wanamlinda nani?Kwanini tumekariri kwamba tunapaswa kuwa na mfumo wa kufanya kazi Mchana pekee? Kwanini Polisi wasisimamie usalama wa vyombo vya usafiri usiku? Hii ni nchi huru tunawaogopa majambazi? Je Mchana hakuna wizi? Viongozi tafakarini, nimeona Tanga, Kilimanjaro na Arusha Mwisho wa safari za abiria ni saa Sita usiku wakati upo uwezekano kabisa wa aboria kusafiri 24hrs, mbona magari hayo hayo hakuna anayekataza kusafiri usiku ikiwa yamekodiwa kwenye majanga mfano msiba? Let us rethink

Soko la karikoo linafanya kazi masaa 14 hadi 16, kwanini wasifanye 24hrs? Tunashindwa kufungua taa na kuimarisha ulinzi wa taasisi za kifedha? Tunatambua kwamba wapo wafanyabiashara wangependa kununua vitu usiku na kusafiri mchana au kununua mchana na kusafiri usiku? Tutawezaje kulipa madeni kama tutaendelea kuishi na fikra za kulala saa kumi na mbili?

Stend ya mabasi mbezi Luisi inafanya kazi mchana tu, kwanini stend kama Ile isiwekewe miundombinu na kutangazwa kufanya kazi 24hrs?
Bar nyingi zinafungwa saa Sita na ukichelewa Polisi wanatinga kuwafurusha au kuwafungia Ndani? Kwanini tusiache biashara watu wajipangie muda wa kufunga na kufungua na kuondokana na mifumo inayohalalisha jambo lililokatazwa Kwa rushwa? Bar tunajua zinafanya kazi 24 hrs na watu wanapewa mpunga kimtindo; kwanini tusiruhusu Hawa walipa Kodi wakala jasho la bila kizingiti?

Mabenki yanafungwa saa kumi, nani kawaambia Mwisho wa kutoa na kuweka fedha ni saa kumi?Hizi mentality za kikoloni tunazitoa wapi?

Najiuliza maswali haya baada ya kuona kwamba wanaotukopesha wanafanya kazi masaa 24 lakini sisi tunafanya kazi masaa nane kisha muda uliobaki tunapumzika. Maana yake sisi tunaraha kuliko wale wanaotukopesha? Lini tutabadilika na kwenda na Kasi ya Dunia?

Ni Lini tutapata watawala wanaoona opportunity kwenye ulimwengu wa kutoa huduma masaa ishirini na nne?

Tumefika mahali hata wagonjwa nao tumeamini wanapaswa kuugua mchana tu, hospitali nyingi usiku zimebaiki na manes na nyingi kufungwa; tumewahi jiuiza tumesababisha vifo vingapi kwa mfumo huu wa kuruhusu huduma mchana pekee nausiku kuona kama ni muda wakulala?Lini tutaona fursa ya kufanya kazi masaa 24 kama njia ya kupunguza tatizo la ajira?

Tunapaswa kuishi Kwa kuangalia matakwa ya wengi siyo wachache
Positive thinking,congratulations.We should rethink again of what kind of country we want to be.It's like we are waiting for the Someone to think and do for us.Poor us!
This Nation need to reform everything including we citizens.
 
Street and Night markets will flourish under strong and committed government instruments,nothing is impossible under the sun except for CCM.
 
Back
Top Bottom