Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Jeshi la Polisi wanapiga marufuku wanafanya biashara ya usafirishaji abiria kufanya kazi masaa ishirini na nne lakini wao wapo kazini masaa ishirini na nne wanamlinda nani?Kwanini tumekariri kwamba tunapaswa kuwa na mfumo wa kufanya kazi Mchana pekee?
Kwanini Polisi wasisimamie usalama wa vyombo vya usafiri usiku? Hii ni nchi huru tunawaogopa majambazi? Je Mchana hakuna wizi?
Viongozi tafakarini, nimeona Tanga, Kilimanjaro na Arusha Mwisho wa safari za abiria ni saa Sita usiku wakati upo uwezekano kabisa wa aboria kusafiri 24hrs, mbona magari hayo hayo hakuna anayekataza kusafiri usiku ikiwa yamekodiwa kwenye majanga mfano msiba? Let us rethink
Soko la karikoo linafanya kazi masaa 14 hadi 16, kwanini wasifanye 24hrs? Tunashindwa kufungua taa na kuimarisha ulinzi wa taasisi za kifedha? Tunatambua kwamba wapo wafanyabiashara wangependa kununua vitu usiku na kusafiri mchana au kununua mchana na kusafiri usiku? Tutawezaje kulipa madeni kama tutaendelea kuishi na fikra za kulala saa kumi na mbili?
Stend ya mabasi mbezi Luisi inafanya kazi mchana tu, kwanini stend kama Ile isiwekewe miundombinu na kutangazwa kufanya kazi 24hrs?
Bar nyingi zinafungwa saa Sita na ukichelewa Polisi wanatinga kuwafurusha au kuwafungia Ndani? Kwanini tusiache biashara watu wajipangie muda wa kufunga na kufungua na kuondokana na mifumo inayohalalisha jambo lililokatazwa Kwa rushwa? Bar tunajua zinafanya kazi 24 hrs na watu wanapewa mpunga kimtindo; kwanini tusiruhusu Hawa walipa Kodi wakala jasho la bila kizingiti?
Mabenki yanafungwa saa kumi, nani kawaambia Mwisho wa kutoa na kuweka fedha ni saa kumi?Hizi mentality za kikoloni tunazitoa wapi?
Najiuliza maswali haya baada ya kuona kwamba wanaotukopesha wanafanya kazi masaa 24 lakini sisi tunafanya kazi masaa nane kisha muda uliobaki tunapumzika. Maana yake sisi tunaraha kuliko wale wanaotukopesha? Lini tutabadilika na kwenda na Kasi ya Dunia?
Ni Lini tutapata watawala wanaoona opportunity kwenye ulimwengu wa kutoa huduma masaa ishirini na nne?
Tumefika mahali hata wagonjwa nao tumeamini wanapaswa kuugua mchana tu, hospitali nyingi usiku zimebaiki na manes na nyingi kufungwa; tumewahi jiuiza tumesababisha vifo vingapi kwa mfumo huu wa kuruhusu huduma mchana pekee nausiku kuona kama ni muda wakulala?Lini tutaona fursa ya kufanya kazi masaa 24 kama njia ya kupunguza tatizo la ajira?
Tunapaswa kuishi Kwa kuangalia matakwa ya wengi siyo wachache