Rais wa Uganda amekaribisha mpango mpya wa maendeleo wa China katika bara la Afrika ambapo Uganda ni miongoni mwa nchi zilizopangwa kunufaika nao
Rais huyo, ambaye alikutana na ujumbe wa China katika Ikulu Ijumaa, alitaja maeneo mawili muhimu ya Uganda ambayo ni kutokomeza umaskini na kuhamisha teknolojia.
Rais huyo alibainisha kuwa serikali yake sasa inaangazia kuwaelekeza watu jinsi ya kutokomeza umaskini katika ngazi ya kaya ili kufikia mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.