Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Viongozi wa Yanga wanaripotiwa kulalamika eti wachezaji wao Niyonzima (Rwanda), Tambwe (Mrundi) na Sherman (Mliberia) "wamezuiwa" kuingiwa Botswana kwa kile wanachodai ni "siasa za mpira".
Huu ni uswahili upande wa viongozi wa Yanga, wala sio siasa za mpira. Suala liko wazi sana, kwamba raia wa Rwanda, Burundi na Liberia wanatakiwa kuwa na visa ili kuingia Botswana. Sasa kama Tambwe, Sheman na Niyonzima hawakuwa na visa walitaka maofisa wa Uhamiaji wa Botswana wawaruhusu kuingia Botswana bila visa kwa kuwa tu wao ni wachezaji wa Yanga? Kumbuka Botswana ni kinara cha utawala bora wa sheria Afrika, viongozi wa Yanga msitake kuleta mambo yenu ya uswahilini mnayofanya huku Bongo. Mnadai hamukuambiwa mapema, kwani mliuliza ubalozi wa Botswana ikiwa hawa wachezaji wangeruhusiwa kuingia bila visa?
Na suala la kusema nyie mliwapokea huku kwetu wakiwa na wachezaji wageni kutoka Zimbabwe mnazidi kujionyesha mlivyo watupu kichwani katika mambo ya kawaida kabisa, kwa sababu raia wa Zimbabwe, nchi ya SADC kama Tanzania, hawahitaji visa kuja Tanzania. Na wala suala la wachezaji wa Zimbabwe kuingia Tanzania bila tatizo sio kwa sababu yenu Yanga. Uhamiaji waliwaruhusu wakijua Zimbabwe wanaingia Tanzania bila visa.
Mnadai mlilipa fedha nyingi kwa ajili ya kina Niyonzima, mnataka kutuambia mlitoa hongo au ada ya kawaida ya visa ya airport? Hela gani kubwa ambayo Botswana watadai kwa ajili ya visa pale airport, dola 50 kwa kila mchezaji? Ndio mnaita hela nyingi?
Na kwa wanachama wa hizi timu kama Yanga, chagueni viongozi ambao wameenda shule kidogo ambao mambo kama haya wanayaelewa sio kuokoteza watu mitaani na kuwapa uongozi kama hawa wa Yanga wanavyojidhalilisha hapa. Viongozi kama hawa wanatutia aibu ugenini.

Tambwe, Niyonzima ‘wazuiwa' Botswana
Gaborone. Andrey Coutinho ana bahati, hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya Amissi Tambwe, Kpah Sherman, Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite kuzuiwa kwa saa moja kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Seretse Khama, mjini Gaborone, Botswana.
Mbrazili Coutinho hakuondoka na wenzake kutokana na kuwa majeruhi wa goti aliloumia katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City mwishoni mwa wiki.
Yanga iliwasili Gaborone saa 4: 35 asubuhi (5:35 kwa saa za Tanzania) na kukutana na kadhia hiyo baada ya wachezaji wake kulazimika kukaa hapo kwa zaidi ya saa wakisubiri suala la wenzao kukamilisha taratibu za uhamiaji.
Wakati wachezaji wakipita katika ukaguzi wa pasi za kusafiria, zile za nyota hao wa kigeni zilionekana na dosari ndogo ambazo uongozi wa Yanga umetamka kwamba walifichwa wakati wakiulizia mambo ya muhimu kuhusu safari yao.
Maofisa hao wa usalama walianza kumzuia Mrundi Tambwe akifuatiwa na Mliberia, Sherman kabla ya kuhamia kwa Wanyarwanda, Twite na Niyonzima.
Maofisa hao walidai kuwa raia hao wa kigeni walitakiwa kuwa na viza za kuingilia nchini humo hati ambazo zilikuwa na msamaha kwa wachezaji na viongozi Watanzania pamoja na kocha Mholanzi, Hans Pluijm.
Kutokana na hali hiyo, mkuu wa msafara wa Yanga kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi akiwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tibohora walimwaga fedha kuwaondoa wachezaji hao katika kizuizi. Akizungumzia hali hiyo, Tiboroha alisema walishangazwa na hatua hiyo ya wachezaji wao kuzuiwa kutokana na awali wakati wanapata taarifa ya nyaraka wanazotakiwa kukamilisha hawakuambiwa kuhusu hayo.
"Hizi ni siasa za mpira, Yanga tumeshangazwa na hili tuliuliza mapema kule katika ofisi zao za ubalozi wa Botswana jijini Dar es Salaam hatukuambiwa kama kuna hili la viza tunatakiwa kulifanya.
Hata wao wakati tunawapokea kule kwetu walikuwa na wachezaji wageni kutoka Zimbambwe, hawakufanyiwa haya, tumelazimika kutoa fedha nyingi ili kuwaondoa wachezaji wetu pale uwanjani," alisema Tiboroha.
Yagomea basi, hoteli
Katika hatua nyingine, Yanga ikiongozwa na makamu mwenyekiti wake, Clement Sanga iligomea basi na hoteli waliyoandalizi wa wenyeji wao, BDF XI kwa kuhofia hujuma.
Sanga ameliambia gazeti hili kuwa jambo la kwanza ambalo uongozi wao uliligomea baada ya kujiridhisha ni hoteli isiyokidhi viwango vya timu yao ambapo wanajeshi hao walipanga timu ifikie katika eneo lisilokuwa na utulivu wa kutosha.
Sanga alisema hoteli waliyoandaliwa na BDF XI ilikuwa imezungukwa na kumbi nyingi za starehe, jambo ambalo alilazimika kuligomea.
Akishirikiana na Watanzania waishio Botswana waliamua kuipeleka timu yao katika Hoteli ya Oasis yenye hadhi na ulinzi wa kutosha.
"Hatukukubali timu ikae pale walikuwa wagumu kukubali wakatuambia wameshalipia, hatukujali tukawaambia kwa kuwa hatujalala ni vyema watukate sehemu ya gharama za usumbufu kiasi kinachobaki watupatie, lakini tungekubali pale tungewaweka wachezaji wetu katika mazingira magumu,"alisema Sanga.
Pia, Yanga ikagomea basi kubwa walilopewa na wenyeji na kuamua kukodi mabasi madogo manne yaliyobeba wachezaji wao wote pamoja na viongozi.
"Hili basi hatutalitumia, tumewaambia tuna usafiri wetu hatutaki kufanya makosa hata kidogo, tunajua mbinu za timu hizi tunataka hili basi kabla ya wachezaji wetu kupanda lifanyiwe usafi maalumu utakaosimamiwa na sisi wenyewe na tukijiridhisha ndiyo tutalitumia," alisema.
Yanga ilitua mjini hapa tayari kwa mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya BDF XI ya hapa, kesho, Ijumaa. Katika mchezo wa awali, vinara hao wa Ligi Kuu Bara walishinda kwa mabao 2-0.
Mwananchi