Viongozi wa Yanga wanaripotiwa kulalamika eti wachezaji wao Niyonzima (Rwanda), Tambwe (Mrundi) na Sherman (Mliberia) "wamezuiwa" kuingiwa Botswana kwa kile wanachodai ni "siasa za mpira".
Huu ni uswahili upande wa viongozi wa Yanga, wala sio siasa za mpira. Suala liko wazi sana, kwamba raia wa Rwanda, Burundi na Liberia wanatakiwa kuwa na visa ili kuingia Botswana. Sasa kama Tambwe, Sheman na Niyonzima hawakuwa na visa walitaka maofisa wa Uhamiaji wa Botswana wawaruhusu kuingia Botswana bila visa kwa kuwa tu wao ni wachezaji wa Yanga? Kumbuka Botswana ni kinara cha utawala bora wa sheria Afrika, viongozi wa Yanga msitake kuleta mambo yenu ya uswahilini mnayofanya huku Bongo. Mnadai hamukuambiwa mapema, kwani mliuliza ubalozi wa Botswana ikiwa hawa wachezaji wangeruhusiwa kuingia bila visa?
Na suala la kusema nyie mliwapokea huku kwetu wakiwa na wachezaji wageni kutoka Zimbabwe mnazidi kujionyesha mlivyo watupu kichwani katika mambo ya kawaida kabisa, kwa sababu raia wa Zimbabwe, nchi ya SADC kama Tanzania, hawahitaji visa kuja Tanzania. Na wala suala la wachezaji wa Zimbabwe kuingia Tanzania bila tatizo sio kwa sababu yenu Yanga. Uhamiaji waliwaruhusu wakijua Zimbabwe wanaingia Tanzania bila visa.
Mnadai mlilipa fedha nyingi kwa ajili ya kina Niyonzima, mnataka kutuambia mlitoa hongo au ada ya kawaida ya visa ya airport? Hela gani kubwa ambayo Botswana watadai kwa ajili ya visa pale airport, dola 50 kwa kila mchezaji? Ndio mnaita hela nyingi?
Na kwa wanachama wa hizi timu kama Yanga, chagueni viongozi ambao wameenda shule kidogo ambao mambo kama haya wanayaelewa sio kuokoteza watu mitaani na kuwapa uongozi kama hawa wa Yanga wanavyojidhalilisha hapa. Viongozi kama hawa wanatutia aibu ugenini.