Viongozi wa Yanga mmetutia aibu huko Botswana

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Viongozi wa Yanga wanaripotiwa kulalamika eti wachezaji wao Niyonzima (Rwanda), Tambwe (Mrundi) na Sherman (Mliberia) "wamezuiwa" kuingiwa Botswana kwa kile wanachodai ni "siasa za mpira".

Huu ni uswahili upande wa viongozi wa Yanga, wala sio siasa za mpira. Suala liko wazi sana, kwamba raia wa Rwanda, Burundi na Liberia wanatakiwa kuwa na visa ili kuingia Botswana. Sasa kama Tambwe, Sheman na Niyonzima hawakuwa na visa walitaka maofisa wa Uhamiaji wa Botswana wawaruhusu kuingia Botswana bila visa kwa kuwa tu wao ni wachezaji wa Yanga? Kumbuka Botswana ni kinara cha utawala bora wa sheria Afrika, viongozi wa Yanga msitake kuleta mambo yenu ya uswahilini mnayofanya huku Bongo. Mnadai hamukuambiwa mapema, kwani mliuliza ubalozi wa Botswana ikiwa hawa wachezaji wangeruhusiwa kuingia bila visa?

Na suala la kusema nyie mliwapokea huku kwetu wakiwa na wachezaji wageni kutoka Zimbabwe mnazidi kujionyesha mlivyo watupu kichwani katika mambo ya kawaida kabisa, kwa sababu raia wa Zimbabwe, nchi ya SADC kama Tanzania, hawahitaji visa kuja Tanzania. Na wala suala la wachezaji wa Zimbabwe kuingia Tanzania bila tatizo sio kwa sababu yenu Yanga. Uhamiaji waliwaruhusu wakijua Zimbabwe wanaingia Tanzania bila visa.

Mnadai mlilipa fedha nyingi kwa ajili ya kina Niyonzima, mnataka kutuambia mlitoa hongo au ada ya kawaida ya visa ya airport? Hela gani kubwa ambayo Botswana watadai kwa ajili ya visa pale airport, dola 50 kwa kila mchezaji? Ndio mnaita hela nyingi?

Na kwa wanachama wa hizi timu kama Yanga, chagueni viongozi ambao wameenda shule kidogo ambao mambo kama haya wanayaelewa sio kuokoteza watu mitaani na kuwapa uongozi kama hawa wa Yanga wanavyojidhalilisha hapa. Viongozi kama hawa wanatutia aibu ugenini.

 
Kwanza unavyosema viongozi Wa yanga wanatakiwa wawe na elimu sijui elimu unayosema wewe ni hipi labda ya mwezini sisi siyo kama Simba

ndugu yangu kwakukusaidia 2 Mwenyekiti wetu kasoma Chuo cha watu vichwa America makamu Sanga ni ingénie huyo Katibu ni mtu mojawapo kati ya Wasomi nchi hii na nimtu Wa mpira sasa usikurupuke tu hoo yanga chagueni Wasomi !!!!

Hizo zi naweza kuwa ni fitna za mpira ili kuwachanganyà wewe hangalia ya kwako unacheza na prison yanga habari nyingine utaumia bure.
 
Mleta mada mwisho ukawaje?young wamelipa fedha nyng ni zao na may b wamelipa kwa kutokujua nini kilipaswa kifanyike,wachezaji waliruhusiwa kuingia nchn botswana?na je watakuwepo ktk mchezo wa kesho?NAOMBA UNIJIBU PLZ.
DAIMA MBELE NYUMA mkiaa
 
sasa wewe na katibu wa yanga nani ameenda shule ya kutosha?hivi ni klabu gani hapa tanzania yenye katibu msomi kama yanga?inawezekana una defn nyingine ya usomi tofauti na inayoeleweka.
 
we kilaza sku nyingine ufiche upuuz wako,yanga kaa nayo mbali,mikia mireeeeefu
 
Mleta mada c bure ww kuna kitu ume2mia b4 kuandika uchafu wako huu!!
 
Wachezaji na viongozi wa soka Bongo hawaishiwi vituko....kuna wale wengine zama zileeeee, walikamatwa wakiiba mataulo kwenye hotelini au kwenye maduka....
 
Mpunga sema ukweli 2 jamaa zetu Simba walifumwa wakiba mataulo usizunguke zunguke kuwa wazi
 
Haya mapenzi niue yanashida yake... Hebu acheni ushabiki wa kijinga. Katika hali ya kawaida unaposafiri nje ya nchi kuna nyaraka za kusafiria kwa abilia yoyote.. Vitu vya lazima ni Passport na Visa. Viza inaweza isitumike kama nchi zinamakubaliano ya kutokutumika kwake.. Ndivyo ilivyo kwa nchi za SADC..

Sasa issue iko wazi Rwanda, Cameroon na Burundi si wanachama wa SADC... Kucheza kwao YANGA haimaanishi wameshakuwa watanzania..

Lazima mkubali uongozi wa YANGA umekurupuka,, na huwezi ukasema eti waliwaachia wachezaji wa Zimbambwe.. Yaan mnataka kutuambia viongozi wa Yanga hawajui kwamba Zimbabwe ni mwananchama wa SADC...

Uswahili wetu tuuachage hukuhuku kwenye soka la bongo!!..
 
Sasa jamani mtu akisema ukweli ndo anakuq mpuuzi.??tatizo walilo nalo yangu lipo pia kwa baba yenu ccm,nyote mmetia pamba maskioni amtaki kuskia ukweli..!!sie yetu macho.!!
 
Yanga wametia aibu ktk jambo hili.hatuhitaji degree kuelewa kitu kidogo kama hiki.huna viza na si mwanachama wa sadc unaenda kufanya nn botswana?vichwa maji sana yanga.
 
mikia wapumbavu sana sijui wivu wa nini sasa sinanyie mchukue ubingwa mkashiriki mnesahau mlishawahi kulala reception na nwenyekiti wenu? kweli mbumbumbu Ni mbumbumbu tu hata ufanyeje huwezi mbadilisha akaelevuka
 
Mimi sio Simba wala Yanga, lakini kwa mtazamo wangu mleta mada kaelezea ukweli mtupu wala si ushabiki, Kuna wakati tunatakiwa tuweke ushabiki pembeni tuukubali ukweli, hata kama jamaa wana madigrii ya Havard kwa hili wamechemka.
 
MFUKUZI;

Kabla ya kulumbana kusiko lazima, tujaribu kujibu maswala mawili rahisi lakini muhimu:

1. Yanga wanaweza kuwa mbumbumbu, sawa. Je, na Kenya Airways nao ni mbumbumbu kubeba abiria wasio na hati halali za kisafiria hadi Botswana kutoka Dar, au na wao pia wanawaogopa Yanga?

2. Je, Botswana haina utaratibu wa Visa on Arrival, yaani kupatiwa Visa baada ya kufika Uwanja wa Ndege?
 
Last edited by a moderator:

sasa wewe na katibu wa yanga nani ameenda shule ya kutosha?hivi ni klabu gani hapa tanzania yenye katibu msomi kama yanga?inawezekana una defn nyingine ya usomi tofauti na inayoeleweka.

Yaani ni afadhali usiwe msomi ukafanya makosa kama haya tutakuelewa. Lakini kama viongozi wa Yanga ni wasomi kama mnavyosema, na bado wanafanya upuuzi kama huu...basi iko kazi, maana Yanga haina viongozi.
 
Yaani ni afadhali usiwe msomi ukafanya makosa kama haya tutakuelewa. Lakini kama viongozi wa Yanga ni wasomi kama mnavyosema, na bado wanafanya upuuzi kama huu...basi iko kazi, maana Yanga haina viongozi.

Hivi uliisoma taarifa yote ya Yanga na nini walifanya kabla ya kwenda Botswana?irudie nadhani utaelewa....!!!
 

Soma vizuri kabla ya kuuliza maswali, habari haijaeleza kwamba wachezaji walikosa hati za kusafiria bali hawakuwa na visa za kuingia Botswana kama utaratibu ulivyo. Kenya Airways haihusiki hapo.
Swali lako la pili, Ndiyo Botswana wana utaratibu wa kutoa visa on arrival.
 
Ulishawahi kusafiri nje ya nchi? Ni shirika gani litalokuruhusu kupanda ndege yake kwenda kwenye nchi ambayo huna viza yake, wala hairuhusu kukupatia viza hiyo utapotua kiwanjani kwao?
 
Ulishawahi kusafiri nje ya nchi? Ni shirika gani litalokuruhusu kupanda ndege yake kwenda kwenye nchi ambayo huna viza yake, wala hairuhusu kukupatia viza hiyo utapotua kiwanjani kwao?

Out of topic, usiulize msikiti Pemba, sasa hivi ninaandika kutoka nje ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…