Viongozi wa Yanga mmetutia aibu huko Botswana

Sasa jamani mtu akisema ukweli ndo anakuq mpuuzi.??tatizo walilo nalo yangu lipo pia kwa baba yenu ccm,nyote mmetia pamba maskioni amtaki kuskia ukweli..!!sie yetu macho.!!

Mkuu ni kweli viongozi wetu walibugi lkn acha kutudhalilisha kwa kutulinganisha na CCM tutukane tusi lolote lkn sio kusema tuna akili kama za CCM hilo tusi linauma mno mtani.
YANGA MBELE DAIMA,NYUMA MIKIA
 
Mimi sio Simba wala Yanga, lakini kwa mtazamo wangu mleta mada kaelezea ukweli mtupu wala si ushabiki, Kuna wakati tunatakiwa tuweke ushabiki pembeni tuukubali ukweli, hata kama jamaa wana madigrii ya Havard kwa hili wamechemka.

Waambie hata Chenge ana degree ya Havard
 
Mbona basi hukujibu swala langu la pili? Au huko unakosema uko umefika kwa ungo?
Swal lako umeuliza Botswana hawana utaratibu Wa visa on arrival umejibiwa wanao utaratibu Wa visa on arrival au usema ulitaka ufafanuzi zaidi,walihitajika kutoa dola 150 kwa ajil ya wachezaj watatu walipotoa wakaruhusiwa hii ndio maana ya visa on arrival
 
Kwa anayefahamu hayo kama wewe, swala la umbumbumbu wa viongozi wa msafara linakosa mantiki, sanasana labda iwe ni ubahili ama ukata. Ila undani wa swali langu umeshaeleweka kwa niliyemuuliza, ameshanijibu na nimesharidhika.
 

Usichanganye mambo!!.. masuala ya viza hayahusiani na Airline. Unaweza ukasafiri na ndege lakini ukaishia Airport..

Wangapi wameshafiri kwenda Marekani au Ulaya na wakarudia Airport!!!?

Sometime ni busara kukubali kwamba kuna sehemu mambo hayakwenda sawa lakini si kuendelea kubishana kisa tu unatetea uongozi wa timu yako..!!
 
Unataka nawe nikuulize kama umeshawahi kusafiri nje ya nchi kwa ndege? Airline gani itayokuchukua bila ya kuwa na Visa au uhakika wa kuipata kwenye airport unayoenda? Wanaorejeshwa airport huwa si kwa kukosa Visa, bali ni utata/kasoro kwenye visa hizo au utaratibu wa kuipata kwa walioahidiwa airport, maswala ambayo ni nje ya uwezo wa airline inayohusika wala Uhamiaji wa kiwanja walivhoondokea.
Kama ni msafiri wa kimataifa, inshalla utakuwa unaelewa pia kwamba mbali ya airline husika, ofisi ya Uhamiaji ya uwanja wa ndege wa kuondokea nayo hawezi kukuruhusu kuuondoka bila ya Visa ya unakoenda au uthibitisho wa kuipata utapofika. Hata ungekuwa sahihi kwamba maswala ya Visa hayahusiani na airline, je hayahusiani na Afisi ya uhamiaji ya kiwanja cha kuondokea? Na kwa hili swala la Visa za Botswana tuseme na Uhamiaji JNIA nao hawakuwa wakijua kazi zao?
Hupaswi kuwa mpenzi wa Yanga, Simba wala timu yoyote nyengine kupata jawabu ya swala hilo.
 
Jerry muro ni majanga matupu..anaongea kama kakalia moto
 

Sielewi unachibishania kwa kweli!!...

Suala la kujiuliza Uhamiaji wa Botswana walikuwa na haki ya kuwazuia wakina Niyozima au la..? Kama ndiyo ni kwanini kama hapana ni kwanini.

Kama wanahaki jibu liko wazi kwamba Uhamiaji wetu ni wamagumashi period!!!

Kuhusu suala la Airline nadhani umeshijijibu mwenyewe... kwamba hata kama wakikubeba mpaka Marekani kama visa yako inamatatizo hawana namna ya kukusaidia utarudishwa tu. So wanaangalia just for formalities tu kuangalia yule anayetakiwa kusafiri ndiye yeye according to your passport na other documents.. Visa ikiwa fake au inamatatizo wao hawasiki utaenda kupambana na uhamiaji..

Naamini umeelewa..!!
 
Wasomi ambao hawafahamu protocol za SADC na nchi ambazo si wanachama wa SADC kama Rwanda na Kenya. Huenda wasomi walipitiwa!
 
Kama hivi ndivyo unavyoamini, maana yake ni kwamba tatizo halikokwa viongozi wa msafara kama mtoa mada anavyotaka watu waamini. Kama ni tatizo, kwa mujibu wa maelezo yako haya, ni la Uhamiaji JNIA. Wenye akili zao timamu hawana sababu ya kuamini hivyo.
 
Ulishawahi kusafiri nje ya nchi? Ni shirika gani litalokuruhusu kupanda ndege yake kwenda kwenye nchi ambayo huna viza yake, wala hairuhusu kukupatia viza hiyo utapotua kiwanjani kwao?
Kama nchi unayokwenda hauitaji viza shirika la ndege hawahusiki mfano mtanzania akienda Hong Kong.
 
Kama nchi unayokwenda hauitaji viza shirika la ndege hawahusiki mfano mtanzania akienda Hong Kong.
Wanahusika kujiridhisha kwamba ni kweli Visa haihitajiki; na kwa maana hiyo ni sawa na kuwa msafiri huyo anayo Visa.
 
Wanahusika kujiridhisha kwamba ni kweli Visa haihitajiki; na kwa maana hiyo ni sawa na kuwa msafiri huyo anayo Visa.
Ha haa haaa! kabla haujakata tiketi lazima wakuulize unakwenda nchi gani.

Kama nchi unayokwenda inaitajika visa hawawezi kukuuzia tiketi mpaka waone visa kwenye pasi yako.

Lakini kama unaenda nchi ambayo hauitaji visa wao wenyewe wanakuuzia tiketi ya nchi unayokwenda.

Kimsingi siyo kila sehemu unayokwenda mpaka uwe na visa mkuu.
 
Labda nawe unisaidie kumwelewesha hivyo mtoa mada na wafuasi wake; hicho ndicho ninachokieleza mimi. Kwamba viongozi wa msafara hawakufanya makosa kuondoka na wachezaji wasio na Visa, madhali imeshathibitika na airline husika pamoja na Uhamiaji wa JNIA kwamba wachezaji hao wangepata visa zao baada ya kufika Gaberone Airport. Tatizo liko wapi?
 
Na kama walijua yote hayo kwa nini walianza kulalamika kwamba wanafanyiwa hujuma na hadi kufikia kuanza kutoa ulinganisho kwamba wao waliruhusu tu pamoja na kwamba kulikuwa na wazimbabwe? hivi hawa Yanga wanahusika na mambo ya uhamiaji kumbe? Na baadaye wakamwaga hela ili waruhusiwe ina maana hao viongozi hawakujua taratibu zikoje?
 

Sasa kwa nini viongozi wa Yanga wanalalamika? Ni dhahiri kwamba walipata viza za wachezaji hao baada ya kulipia (japo wanalalamika 'kumwaga' fedha). Nikisoma malalamiko yao ni kwamba wanahoji ni kwa nini walazimishiwe viza ilhali ni wachezaji wa Yanga? Wanajaribu kulinganisha wazimbwabwe na warundi/wanyarwanda. Kumbuka hawakuzuiwa ila walitakiwa kufuata taratibu za viza....

Huyu kiongozi aliyelalamika hana uelewa wa taratibu za uhamiaji.
 

Umepanic ww, aibu wamekutia ww na ndugu zako, mashabik sisi shangwe tu nw twaenda hatua nyingne hatunahabar sis
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…