Hizo ni tafsiri zako kwa mujibu wa walivyoripotiwa viongozi hao. Lisilopingika ni kwamba hakukuwa na tatizo kwa wachezaji hao kuondoka Dar bila ya Visa, wala hakuna tatizo kwa wachezaji hao kutakiwa kulipia Visa Gaberone. Mtoa mada aliyataja hayo kuwa ndiyo kiini cha udhalilishaji aliouzungumza. Wewe unahisi kwamba udhalilishaji ni kwa viongozi kufananisha Wazimbabwe wa BDN na Warundi, Waliberia na Wanyarwanda wa Yanga. Naweza kukubaliana nawe iwapo itathibitika viongozi hao wamefanya hivyo, ingawa hiyo ni mada tofauti. Siwezi kukubaliana na mtoa mada kwa sababu kasoro ya dhana yake iko kweupeni, haihitaji tochi!