Viongozi wadini waumini awapendezwi kuona wanasiasa wanaingia kwenye mimbari, tuwakataze

Viongozi wadini waumini awapendezwi kuona wanasiasa wanaingia kwenye mimbari, tuwakataze

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Huu mfumo wa viongozi wa serikali kuongizwa kwenye ratiba ya misa unaligawa Taifa. Haiwezekani kila siku tukahutubiwa kupitia dhehebu moja kwa sababu tu kiongozi flani ametoka dhehebu ilo. Kwamba kiongozi akiwa mkatoliki kila jumapili anakwenda kuzungumzia kanisani, akiwa Muislam tumsikilize msikitini, akiwa mlutheri tunakae kwenye tv kufuatilia misa za Lutheran? Hapana, huu utaratibu tunapaswa kuukataa, huu utaratibu wa tv kwenda kanisani kila jumapili na msikitini kila ijumaa tunapaswa kuupiga Vita.

Viongozi wa siasa acheni mamlaka zenu nje, ingieni kwenye ibada kama waumini msinajisi na kuwakwaza wahumini wasiokubaliana na sera au approach zenu.

Nyumba za ibada zibaki kuwa nyumba za Ibada na majukwaa ya siasa yatumike kwa ajili ya siasa. Taifa haliwezi kuhutubiwa au Watumishi wa Umma awawezi kupewa maelekezo kutoka kenye nyumba za ibada. Katiba inakataza, tutenganishe majukumu ya serikali na kisiasa na imani
 
Back
Top Bottom