uchumi2018
JF-Expert Member
- Mar 4, 2018
- 2,085
- 2,996
Salaam wakuu,
Imenibidi niingie uringoni kutoa mawazo yangu kuhusu harakati za uchaguzi mkuu ulioko mbele yetu.
Binafsi naamini hakuna jambo zuri lisilokuwa na upinzani. Binafsi naamini hoja ya NO REFORMS NO ELECTION imepitia vikao na ngazi zote za chama na kuangalia mazuri na mabaya yake na kuangalia namna ya kuyakabili.
Si busara mtu yeyote wa ngazi yeyote kwenye uongozi wa chama kuibuka na hoja nyingine tofauti na hii.
Maadam watanzania tumewaelewa, tunaomba msiyumbishwe na mawazo mbadala mengine yanalenga kuwagawa ili kuwakwamisha.
Kuhusu kundi linalojiita G55, mimi binafsi naona wapewe nafasi au ya kubaki kwenye chama waunge mkono hoja iliyopo mezani,au wapewe uhuru wa kujiunga na vyama vingine. kuondoka kwao kutaacha nafasi ya wengine kujiunga na chama,kuliko kuwa na upinzani wa ndani ambao ni hatari ya maendeleo.
Ninawatakia kutafakari vyema, watanzania wengi tumechoshwa na maigizo ya chaguzi, tuanatamani kuwa na chaguzi zenye maana ili anayeshinda ashinde kwa haki na watu wote tuiopo pembeni tuseme uchaguzi ulikuwa wa haki.